Nilikuwa na mpenzi niliyempenda sana , ila juzi nilimpigia simu akadai yuko kazini akaniambia akitoka ataniambia. Baada kama masaa mawili akanipigia simu akaniambia tukutane mahali fulani muda fulani nikamjibu sawa , baada kama lisaa limoja tena akatuma text akisema bby tuonane kesho, nikajibu ok kwa shingo upande mimi nikarudi nyumbani na usiku ulikuwa umeingia.
Badae nikapiga simu yake haipatikani , nikatuma txt nahisi unanicheat kwanini unizimie simu? ok me nikaingia kulala.
Saa tisa usiku nikapigiwa simu kupitia simu ile ya mtu wangu ila aliyeongea sio yeye aliongea mtu jinsia sawa na mimi kwa kutumia simu ya mtu wangu akiniuliza we ni nani unayemtumia mtu wangu txt nikamjibu muulize huyo uliyenaye mimi ni nani kwake. Sikuweza kuongea kwa ukali maana nilikuwa na mtu jilani yangu (ndugu yangu ambaye nalala naye chumba kimoja) akakata simu.
Nikatoka nje ili ni mpigie niongee naye huyo mtu aliyenipigia simu kupitia simu ya mtu wangu ile simu hakupatikana tena, mchana akanipigia huyo mtu wangu sikuweza kupokea maana nilikuwa na hasira sana akatuma txt ya KUOMBA msamaha sikujibu chochote , leo nimempigia simu nikimuomba tukutane sehemu flani ila hajaja baada ya mimi kuondoka anapiga simu nikasema nimeondoka akasema poa.
Naombeni ushauri wakuu na mimi nijifanye mjinga nimsamehe ili nami nilipize kisasi au nimsamehe tu niendelee naye au nimpige chini niachane naye kabisa? Au wewe unashauri nini?