Kupelea

L'AMOUR

Senior Member
Mar 8, 2011
110
24
Jana nimesikia mtu akisema maji ya kumwagilia yamepelea, kuingia kwenye daladala nako mtu anamsimulia mwenzie kuwa alishindwa kununua kitu hela ilipelea. Sasa hapa nawiwa na maneno ya kueleza ni wapi hasa kupelea inatumika je ni kwa vitu vinavyohesabika au visivyohesabika na vipi kama inatumika kwa vyote? Kama inatumika kwa vyote je tunaweza kusema kuwa umri wa mtu umepelea kwa miezi kadhaa ili aweze kuruhusiwa kupiga kura?
Tafadhali wanaJF
 
Mkuu umri wa mtu hauwezi kupelea hata siku moja kwa vile hawezi kuongeza miaka yake.
Mfano: Chukua mwaka uliozaliwa (i.e 1989) halafu jumlisha miaka yako hadi leo (22yrs). Je umepata ngapi? lazima utapata mwaka 2011. ukijionezea miaka hutopata huo mwaka. Fanya hiyo hesabu kwa wadogo zako wote lazima jibu ni moja.
Pia unapo tumia neno "pelea" elewa kwamba kuna kujazilizia au kuongezia kwa kilicho pungua. Kwa kingereza ni "replenish".
 
Kupelea ama pelea ni msamiati unaotumika kuonyesha kutokutimia kwa idadi lengwa, la kuzingatia ni idadi lengwa, na neno hutegemea neno jingine ili kutoa maana.
 
Back
Top Bottom