Kupatwa kwa jua na yanayotokea sasa Tanzania

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Habari za jumapili wakuu!

Mwaka 2016 kila mtu anakumbuka kulitokea tukio la kihistoria nchini, kupatwa kwa jua kulipata kuonekana kwa asilimia kubwa nyanda za juu kusini mkoani Mbeya Tanzania.

Baada ya tukio hilo kubwa duniani, ilifuatiwa na tetemeko lililoleta maafa makubwa mkoani Kagera,

Na kwa kipindi hiki tukio lililofuatia ni ukame na Njaa.
hali ya hewa nchini imekua ya tofauti sana jua limekua kali kila kona ya nchi, na ukame umetawala hali inayotishia usalama wa binadamu na mifugo kwa kukosa chakula na maji.

Wajuvi wa mambo Jf, hivi kunauwezekano wa tukio la kupatwa kwa jua na kutokea kwa Tetemeko?

pia kutoweka kwa mvua na ukame kutamalaki nchi nzima inawezekana ni kutoka na kupatwa huko kwa jua?

Nawasilisha.
 
Havina uhusiano wowote!
Magu ashapiga chini michango ya maafa kagera

Serkali haina shamba pia nani kasema kuna njaa nchini?
 
Nchi imekosa waombaji wamebaki walalamishi tu,zamani kama mvua imegoma watu maalumu walikua wanaenda kwenye masinagogi ya kiafrika kuomba,kwenye miti,mapango,mawe n.k...na mvua inanyesha au janga linapungua,leo hii watu wamebaki kulalamika tu,waombaji ni wasanii tu,wanajifanya ni wa MUNGU lakini ni wana mambo ya dhambi,MUNGU atawasikia?kwa mfano hakuna waombaji wazuri wakakaa ndani kumlilia MUNGU kama wanawake na MUNGU akajibu,lakini wanawake hao waombaji wako wapi?kila kukicha wanabana maungo yao na nguo za aibu,kila kukicha ni ugomvi wao na wanaume tu wakidai pesa,waombaji wako wapi?majanga haya wakati mwingine tumemkosea MUNGU sana ndo mana anatuacha.kupatwa kwa jua na kukosekana kwa mvua havihusiani,kinachotokea ni kupatwa kwa dhambi na matetemeko ya tabia.tubadilike tuwe wasafi wa roho na mwili
 
Mungu amechukia Ccm walivyoiba kura.Allah anachukizwa na utawala huu ndio maana mvua katunyima
 
Wachache watakuelewa ulicho kiwasilisha!!

Tatizo ni ukosefu wa maadili ktk jamii, watu hawana hofu ya mungu.
Watu tunaishi kama wanyama, hatuendi makanisani wala misikitini, maovu ya kila aina yamekithiri ktk jamii zetu.

Natural disasters kama vile; mafuriko, matetemeko ya ardhi ukame, kupatwa kwa jua n.k yote haya ni matokea ya matendo maovu yaliyo kithiri ktk jamii.

Hakuna takaye salimika uwe mchamungu au muovu kama hatutotumia nguvu kukemea maovu ktk jamii zetu husika, anza na familia yako iwe ni familia yenye kumjua mungu.
Sote tumuombe mungu atuepushe na majanga, hakuna wa kumnyooshea kidole mwenzake, hakuna aliye kamilika.
 
Umesema kweli mkuu, hapa lazima tumrudie muumba wetu tu!

Tulipofikia sasa si pazuri kwakweli
 
Nchi imekosa waombaji wamebaki walalamishi tu,zamani kama mvua imegoma watu maalumu walikua wanaenda kwenye masinagogi ya kiafrika kuomba,kwenye miti,mapango,mawe n.k...na mvua inanyesha au janga linapungua,leo hii watu wamebaki kulalamika tu,waombaji ni wasanii tu,wanajifanya ni wa MUNGU lakini ni wana mambo ya dhambi,MUNGU atawasikia?kwa mfano hakuna waombaji wazuri wakakaa ndani kumlilia MUNGU kama wanawake na MUNGU akajibu,lakini wanawake hao waombaji wako wapi?kila kukicha wanabana maungo yao na nguo za aibu,kila kukicha ni ugomvi wao na wanaume tu wakidai pesa,waombaji wako wapi?majanga haya wakati mwingine tumemkosea MUNGU sana ndo mana anatuacha.kupatwa kwa jua na kukosekana kwa mvua havihusiani,kinachotokea ni kupatwa kwa dhambi na matetemeko ya tabia.tubadilike tuwe wasafi wa roho na mwili
Manabii wamekuwa wengi sana..labda ndio Mungu kaamua kutuchapa kwa style hii mkuu
 
Back
Top Bottom