Mi nina namba 3, namba 2 wanazijua wote na head wa kazini akiwemo. Namba hizi zinajiwasha saa 0600 na kujizima saa 2200.
Namba 1 hii haizimwi kabisa, inajulikana kwa wanafamilia wote, marafiki wa karibu, wafanyakazi wawili tu tunaofanya nao kazi na ndio namba nimeunganisha kwenye huduma zote za kibenki.
Siku nikiamua nisipatikane sipatikani kweli. Sio umeamua usipatikane ukaamua kuzima simu, bahati mbaya umepata dharura unawasha simu ili utoe hela mpesa, mara bosi anapiga simu tena, yaani kama alikuwa anakusubiri wewe.
Utaratibu huu nilijifunza nilikuwa na bosi mmoja msumbufu sana, nikaona nikimzimia simu yeye watu wengine tuendelee kuwasiliana kama kawa.