Kupatikana masaa 24 ni u-cheap labour

Kupatikana masaa 24 ni u-cheap labour

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,556
Reaction score
63,025
Mawasiliano ni kitu cha muhimu sana.Lakini si vizuri kwa masaa 24 kila mtu anayekutafuta awe anakupata kwenye mawasiliano.Ile hali ya mtu yeyote kukupata masaa 24 tunaita ni u-'cheap labour'.Yaani wewe unajiweka cheap katika maisha yako.Anayetakiwa kukupata wewe masaa 24 ni mke/mume,watoto,wazazi wako.Kuhusu marafiki,mabosi zako kazini n.k wanatakiwa wawe na limit kwenye muda...mfano mwisho wa mawasiliano yao uwe ni baada ya kutoka kazini n.k.Baada ya hapo simu /laini inakuwa off...hii itakupa heshima na kila mtu atakuona wa thamani.Si sifa bosi wako kukupigia muda anaotaka..mfano saa nne usiku au usiku wa manane...ukiona hivyo ujue wamekuona wewe ni 'cheap'. Unaweza kuwa na mtandao/laini kwa ajili ya kazi,marafiki,familia..Ni mtazamo wangu.....
 
Hi inawahusu walio ajiriwa tu, sisi tuliojiajiri haituhusu, coz 24/7 tupo hewani
Ni kweli mkuu,ila unaweza kujiwekea utaratibu ni nani na kwa muda gani akutafute,ukiwa na simu ya biashara na nyingine ya maisha yako mengine.
 
Unazingua some time kunakuwa na issue muhimu na inategemea na kazi unayofanya ww
ha ha ha ha,kabla ya kuajiriwa wewe si walikuwepo wengine kabla yako,wako wapi sasa?Heshimu muda wa kazi na upatikane muda wa kazi...itakupa thamani.Tofauti na hapo utaonekana 'cheap'
 
Hii ina wahusu wajasiliamwili....?
ha ha ha ha inawahusu wote mkuu,kuchuja ni muhimu,ni nani akupate masaa 24 na ni kwa ajili ipi.Furaha ya nafsi na amani ni muhimu zaidi.
 
Mi nina namba 3, namba 2 wanazijua wote na head wa kazini akiwemo. Namba hizi zinajiwasha saa 0600 na kujizima saa 2200.
Namba 1 hii haizimwi kabisa, inajulikana kwa wanafamilia wote, marafiki wa karibu, wafanyakazi wawili tu tunaofanya nao kazi na ndio namba nimeunganisha kwenye huduma zote za kibenki.
Siku nikiamua nisipatikane sipatikani kweli. Sio umeamua usipatikane ukaamua kuzima simu, bahati mbaya umepata dharura unawasha simu ili utoe hela mpesa, mara bosi anapiga simu tena, yaani kama alikuwa anakusubiri wewe.
Utaratibu huu nilijifunza nilikuwa na bosi mmoja msumbufu sana, nikaona nikimzimia simu yeye watu wengine tuendelee kuwasiliana kama kawa.
 
Back
Top Bottom