Kupatikana Kwa Muafaka Na Amani Arusha Uchaguzi Wa Umeya Urudiwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kupatikana Kwa Muafaka Na Amani Arusha Uchaguzi Wa Umeya Urudiwe!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ndallo, Jan 8, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,136
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  Kitendo kilichojitokeza katika jiji la Arusha kuchafuka kutokana na vurugu za kisiasa kati ya wananchi na polisi yote haya ni kulazimisha ushindi usiokubalika na wananchi wa leo Tanzania kutokana na sasa kila Mtanzania aliyefikisha umri wa kupiga kura anajua haki yake ya msingi ya kumchagua na sio kumchagulia kiongozi asiekubalika katika jamii hii ya leo ndani ya nchi hii. Narudia tena ile kauli ya aliyekua waziri mkuu kwenye serikali ya awamu ya kwanza raisi akiwa baba wa taifa (Mungu amrehemu na amuweke mahali pema peponi) muheshimiwa Joseph Sinde Warioba alihawahi sema nanukuu: WATANZANIA NI WAPENDA AMANI SANA NA WASIZARAULIWE! NA SIKU WATAZARAULIWA ITAFIKA SIKU WATASEMA BASI! mwisho wa kunukuu. Sasa natumaini watanzania wameshaelewa usemi huu wa kiongozi huyu katika taifa hili na tumeshayaona na yametokea kuanzia kumalizika kwa uchaguzi mkuu hadi hapo majuzi watu hadi kupoteza maisha na huu naona ni mwanzo tu endapo serikali iliyopo madarakani haitawasiliza wananchi ni nini wanataka au wanataka kiongozi gani kweli damu za watu wasiokua na hatia itaendelea kumwagika na ile sifa aliyotuachia baba wa taifa itatoweka na nnchi hii kupoteza ile sifa ya Tanzania ni nnchi ya amani. Ili muafaka na amani irudi tena Arusha hakuna budi CCM na CHADEMA kurudia uchaguzi wa Umeya ili haki ipatikane na atakayeshindwa ayakubali matokeo na sio kulazimisha. Natanguliza hoja hii mbele yenu enyi wapenda amani.
   
 2. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Absolutely right,na hatutaacha mpaka kieleweke
   
 3. l

  leonews New Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  CCM na serekali wanapaswa kutambua kwamba Amani haitakuwepo kamwe kama haki haitatendeka. Na vilevile watambue kuwa amani hailetwi na mtutu wa bunduki. Uchaguzi urudiwe na uwe huru na wa haki amani iwepo. Meye uliepachikwa Mr Gaudence Lyimo washauri wenzio tupate amani Arusha.
   
 4. l

  leonews New Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hii ni kweli kabisa
   
 5. D

  Discoverer Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Damu ya watu iliyomwagika Arusha itakaa mikononi mwa ccm kwa kipindi chote hiki cha miaka mitano.
  Na hii itali cost taifa, inabidi uongozi huu dhalimu ung'olewe madarakani kabla ya kuisha hiki kipindi
  mimi sio mtabiri, lakini tujiandae kwa miaka mitano ya kulia na kusaga meno.
  Anaeunga mkono CCM anaunga mkono umwagaji wa damu uliopindukia.
   
 6. kalagabaho

  kalagabaho JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,267
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  hayo ni mawazo potofu kudhani kuwa Arusha inawakilisha watanzania wote
   
 7. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Kilichotokea Arusha lazima CCM na serikali yake wakemewe na watu wote wenye mapenzi mema na taifa la Tanzania hata kama upo CCM,CDM,CUF,TLP na hata kama huna chama.kama hautafanya hivyo basi utaungana natutakuita fisadi/mafisadi wa serikali kama DOWANs,Richmond,Meremeta na mengine ambayo bado hatujayajua  KATIBA INAHITAJIKA TENA HARAKA SANA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU NA TUNAMWOMBA HUYO MEYA WA ARUSHA AJIUZULU MARA MOJA AACHE UCHU WA MADARAKA MAANA HAPAKALIKI HAPO ARUSHA LAZIMA KIELEWEKE TU
   
 8. h

  hamida ally Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  real that is solution
   
Loading...