Kupata mikopo toka Benki

BelindaJacob

Platinum Member
Nov 24, 2008
6,474
4,022
Habari,

Inawezekana kupata mikopo kwa shughuli muhimu kama kujenga nyumba kwa mtu asiyefanya kazi?
Nini kinatakiwa kwenye mlolongo wa kupata mikopo zaidi ya hati ya nyumba kama itahitajika? na kama inawezekana, benki gani inaweza kuwa na riba nzuri?
 
Kwa benki za hapa Bongo kama hufanyi kazi sio rahisi kusikilizwa achia mbali kupewa mkopo. Kuna baadhi ya benki siku hizi hati za nyumba za kawaida wanagoma,labda kama ni nyumba ya biashara wanakubali. Kwa hiyo dhamana ni lazima.Kama una dhamana ya kuaminika nenda Twiga Bancorp pale, wale riba yao nafuu kidogo. Kama ni mwajiriwa basi ndani ya siku saba kitu tayari, ili mradi mwajiri wako awe tayari kukupa support kwanza kwa kupitishia mshahara wako kwao.

Vinginevyo, ukiwa na sifa hizo jaribu akiba commercial bank wako vizuri pia.
 
sijui kama mkopo unaweza kutolewa kwa mtu asie na biashara wala mfanyakazi!labda mnisaidia kwa hili
 
Ney,

Huna kibarua,huna biashara au dhamana yo yote ile huwezi kupata mkopo wa benki, labda nikukopeshe za kwenye kibubu changu !!!!!!
 
Hapa kwetu hati ya kiwanja au nyumba havina thamani hadi kuwe na uthibitisho wa ajira au biashara. Mimi nimeenda benki zote nikiwa na hati ya kiwanja nikakosa tena pesa ndogo tu milion tano wakati kiwanja thamani yake ni milion kumi. Kwa hili benki zetu hazitusaidii kabisa
 
Back
Top Bottom