Kupata kazi au cheo bila ‘connection’ sahau

Kupata kazi au cheo bila ‘connection’ sahau

Wakuu.

Hii nchi ngumu sana , tamu sana !

Yaani kazi yoyote ile kuipata bila connection ni kazi sana. Yaani lazima mtu akudokeze , akusukume , akuunganishe au fitina lazima ifanyike.

Unakuta kazi kabla haijatangazwa tayari wenye ndugu wanajua na wameshatambulishwa mahali! Kuita watu Interview toka Mikoani ni dhambi kubwa sana.

Unawaita watoto wa watu wanajichanga huko mikoani wanasafiri mpaka mjini kwa shida.

Wanaingia interview wakati kazi watu wamepewa. Kijana wa watu anarudi kijijini kwa taabu sana.

Tanzania kazi kabla hata haijachapishwa kwa gazeti , watu wameshasubmit vyeti.

Hovyo sana sekta ya ajira.
Wakati enzi za mwaalimu mlikuwa mnachagua kazi jeshini ndio kabisaaaa wasomi walikuwa hawataki hata kusikia sasa hivi ebwanaeee na wenye master zao wanapigana vikumbo heshima imerudi kwa kweli shikamoo Magu
 
Mkuu cpnnection tutaipataje sasa sisi wengine Mkuu.Tupe mbinu basi za kupata connection
 
Wakati mwingine hii dunia inafikirisha sana hadi Mtu unajikuta ukitenda dhambi za making'uniko rohoni bila hata kukusudia.
 
Sio kazi tu, kila kitu. Hadi mume/mke unahitaji connection
 
Wakuu.

Hii nchi ngumu sana , tamu sana !

Yaani kazi yoyote ile kuipata bila connection ni kazi sana. Yaani lazima mtu akudokeze , akusukume , akuunganishe au fitina lazima ifanyike.

Unakuta kazi kabla haijatangazwa tayari wenye ndugu wanajua na wameshatambulishwa mahali! Kuita watu Interview toka Mikoani ni dhambi kubwa sana.

Unawaita watoto wa watu wanajichanga huko mikoani wanasafiri mpaka mjini kwa shida.

Wanaingia interview wakati kazi watu wamepewa. Kijana wa watu anarudi kijijini kwa taabu sana.

Tanzania kazi kabla hata haijachapishwa kwa gazeti , watu wameshasubmit vyeti.

Hovyo sana sekta ya ajira.
"Nahuyo wa bush akipata hiyo ajira next time anawakonect ndugu zake and the cycle repeats"
 
Hapa Nakubaliana nawe kwa asilimia chache sana, kwasababu mimi Mwenyewe niliwahi kupata kazi sehemu fulani hivi bila kuwa na mtu wa kuniunganisha. Kinachomata siku hizi ni Ufaulu.
 
Haya mambo yalianza zamani. Miaka ya 1990 nilipata scholarship ya serikali (Wizara ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa na Ben Mkapa wakati huo). Ukitoa viongozi wa juu wa Wizara, wengine wengi wao walikuwa Wazanzibari. Kuna jamaa akiitwa Fitawi na mwingine Shaban. Wala rushwa wakubwa sana. Basi majina ya scholarship yalipotoka, jina langu lilikuwemo. Nikafurahi lakini pia nikawa nashangaa kuwepo bila kutoa rushwa. Ilikuwa ya kwenda kusoma udaktari Urusi. Wakati wa kuondoka, jina langu lilikwisha tolewa. Nilijaribu kwenda kumwona Mkurugenzi wa Elimu ya Juu lakini haikusaidia. Kila niliyemwona, alikuwa anawatetea akina Shabani na Fitawi. Nikagundua kuwa hii ni kesi ya tumbili... Nikaishia kusoma Tanzania. Lakini baadaye nilimshukuru Mungu sana kwa kusoma Tanzania. Tanzania ni miaka 5 tu nikawa nimemaliza. Waliokwenda Urusi walichukuwa miaka 7-8 kumaliza. Waliporudi, walinikuta mimi tayari ni chief wao. Kwa hiyo nami naweza kupigiwa simu siku moja ili nihesabiwe kama niliyesoma Urusi. Mpaka leo ninayo barua ya Wizara ya kwenda kusoma Urusi.
Same page of the story different books. Tuko wengi omusolopagasi
 
Back
Top Bottom