One Means Together
Member
- Jul 21, 2014
- 15
- 8
Hata mimi nimepatwa na hilo ndugu,risiti ninayo ila wameishusha bei tofauti na nlivyonunua. Wakaniambia tu tunaomba hivyo ili makato kwetu yasiwe makubwa!!!!! Nikashangaa.Mkuu kama imeshindikana kupewa kadi ambapo ni zoezi la siku moja tu kuhamisha umiliki kutoka kampuni muuzaji kwenda kwa mteja mnunuzi.
Sitarajii kama huyo muuzaji atakuwa muadilifu kutoa risiti ya EFD yenye thamani ya Million 3+ tena inayosoma bidhaa halisi iliyouzwa na sio risiti ya kutembelea asisumbuliwe na askari.
Wameandika chasis number, wakaniambia kadi na plate number ni baada ya wiki 2. Hii wiki ya kwanza nimemaliza leo. Lakini hii ya kadi ntapata baada ya hizo wiki mbili imekaaje wakati wengine vitu vyote wanafanya ndani ya siku tatu. Sijaelewa hapo. Naweza kushtaki vipi? Na je, mtandaoni naweza kuangalizia kwa wapi ili nione tu kama chasis number inasoma ya usajili wa jina langu!! Nina risiti na TIN number