Kupanda kwa mafuta na fursa ya matumizi ya rasilimali zetu

Singo Batan

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
292
191
Tanzania kama Nchi nyingine kwa sasa imekuwa miongoni mwa mataifa yaliyokumbwa na maumivu ya kupanda kwa Mafuta na gharama za maisha.

Hii kwa upande mwingine yaweza kuwa chachu ya ubunifu kuhusu mbadala wa matumizi ya nishati hii inayotufanya kuwa Watumwa.

Mathalani tunayo gesi, ni wakati sahihi sana kutumia wataalamu wetu walioonesha uwezo wa kubuni na kuinstall mifumo ya gas katika vyombo vya usafiri (Mf. DIT).

Pamoja na changamoto za umeme lakini ingefaa sasa kuwekeza katika uundaji wa vyombo vya usafiri vinavyotumia umeme (kuwawezesha Kina Masoud Kipanya na kasi ya magari ya umeme).

Vituo vya mafuta ingefaa vibadilishwe na kuwa vituo vya NISHATI (umeme, gas na mafuta).
Tukifanikiwa hapa tutakuwa tumefaulu kwa kiasi kikubwa kujiepusha na rungu la OPEC plus dhidi ya watumiaji wa mafuta duniani kote.
 
 
Back
Top Bottom