Kuoza Meno Kunavyo Watesa Wadada Mjini

666 chata

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
1,710
Reaction score
4,046
Kwa wanaume ni kawaida au tuseme imezoeleka tu kawaida kukuta huyu ana mapengo, huyu ana meno ngiri, huyu ana meno ya njano sanaa, huyu meno yake yamearibiwa na wadudu, na vyote hivi jamii haishangazwi sanaa, maana kundi hili bhana mtu anaweza kuondoka mzima akarudi hana meno, ni kawaida hawa, wana mengi hawa na japo inategemeana mtu na mtu, wale wa uswahilini wanakwambia "Mwanaume Mashine".

Tatizo lipo kwa kundi hili la wanawake, wasichana, warembo, mabinti, kundi hili bhana linachukuliwa tofauti kidogo, na ni wazi kundi hili ni mapambo au maua ya ulimwengu, ndio maana hua sishangai nikiona bibi kizee kikongwe kabisa kapaka wanja nae au ana upara kiujana jana hahah, sasa tatizo kubwa siku hizi na linalokua sanaa kwa kasi la hawa wanawake wa leo la "Kuoza Meno" tena yale meno ya mbele kabisaa.

Unakutana na binti wa maana mzuri kweli lakini akicheka daah utamuhurumia yaani vijimeno vya mbele vinaweusi kwa ndanii, wadudu wamekula, na ugonjwa huu ni kama umeshamiri sanaa, unakuta mtu tujino twa mbele tumeliwa na wadudu na tumekatika au tuna weusi yaani tabu sanaa.

Najua jambo hili lina watesa wengi na kuwafanya wakose kujiamini sanaa mbele ya jamii hasa zikija habari za kufurahi na kusmile vile vile, si ajabu basi wakawa wanajiona ni ma vampire au zombie, lakini kama jukwaa naamini hakiaribiki kitu, kama kuna dawa basi ijulikane iwekewe wazi au kama kuna namna basi ijulikane.

Vingine kama precautions tu ni vyema tukatafuta nyuzi za mfano wa mshipi ambapo kila tukimaliza kupiga mswaki basi tuwe tunazipitisha kwenye meno yetu ilikuondoa mabaki ambayo mswaki haufiki kule, na tusipendelee sanaa kula vitu vya sukari sukari nyingi kama chocolate na biskuti sanaa sanaa kwakua moja ya matokeo yake ndo kama haya.


NB: vitu vidogo vidogo ndio vinatupa furaha, na vitu vidogo vidogo hivi ndio vinaweza kutunyima furaha kubwa ktk maisha yetu.
 
Hahaha......mm yangu yamechanganya
 
Mm mwenyewe na jino lilipasuka nilikuwa napenda sana kutembea na toothpick mdomoni, nikawa nalichokonoa mpk likapauka, basi hapa navyoandika linauma hataree, siyo LA mbele lkn
 
Hili tatizo hutokana na madini Fulani ya fluoride kuzidi kwenye MAJI na mhusika huanza kupata tatizo hili wakati meno ya ukubwani yanaanza kuota. Inategemea MTU alikulia wapi na MAJI yakoje. Hili tatizo kubwa sana SINGIDA na ARUSHA. Ushauri ni kuwa serikali yetu tukufu iboreshe huduma za MAJI ili MENO yapendeze kwa wanaokuwa.
 


Mkuu, nazungumzia meno mazima ambayo yamekuja kuaribika ukubwani, na sio rangi ya meno tokana na maji chumvi.
 
Hili tatizo liko Arusha na Singida hasa eneo wanapoishi kabila la Wanyiramba
Arusha huwa wanasema ni maji yana calcium kwa wingi ...
Ila mimi nimezaliwa na kukulia hapa hapa Arusha, But sijawa na meno mchuzi..[emoji1]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…