Kuosha maembe kwa sabuni

Bree ven

JF-Expert Member
Apr 11, 2013
375
363
Naomba kuuliza wataalamu, kuna tatizo lolote iwapo mtu anaosha maembe kwa kuyasafisha na sabuni kisha kuyasuuza vizuri kwa maji safi na kisha kula maganda yake?
 
Hata nyanya, vitunguu, karoti, maparachichi, mapera, mapapai, miwa, matango n.k unaweza kuisha kwa sabuni!
 
Mkuu haina madhara, tatizo itategemea na harufu ya Sabuni itakayobaki katika embe lenyewe.

Huenda ukaikosa ile ladha haswaa alafu pia ukishakula embe lako ile harufu ya Sabuni ikabakia mdomoni au kooni! Huenda ikasababisha kichefu chefu.

Sioni sababu ya kuosha kwa sabuni, tumia maji ya kawaida tu kuliosha vizuri. Ama kama kuna ulazima wa kufanya hivyo, tumia sabuni ya mche wa Jamaa isioacha harufu. Epuka sabuni ya Unga na sabuni za mikono yaani Hand Wash Soap.
 
Sioni kama ina tatizo mkuu. Ila nadhani itabidi uangalie aina ya sabuni, usije ukaosha kwa rungu medicated soap
 
Kuosha na sabuni inawezekana ila uwezekano wa residual kubaki ni mkubwa.

JIK ni nzuri zaidi. Weka 1 part JIK, kwenye 3 parts water halafu rinse.

Alternatively, hata hydrogen peroxide inafanya hiyo kazi. Lakini tumia ile ya mouth wash ambayo nadhani ni 3% na uchanganye na maji.
 
"Kutokana na matumizi ya madawa ya kuulia wadudu kwenye mimea ya matunda na mbogamboga inashauriwa kutumia detergent isiyo na kemikali yenye madhara ili kuondoa sumu hizo kwenye vyakula hivyo" Mimi huwa natumia pia sabuni ila natumia maji mengi sana kwa kusuuza
 
Unashauriwa uyaloweke kwanza na sabuni ya unga mda wa siku 2 ndio Mambo mengine yafuate
 
Mkuu haina madhara, tatizo itategemea na harufu ya Sabuni itakayobaki katika embe lenyewe.

Huenda ukaikosa ile ladha haswaa alafu pia ukishakula embe lako ile harufu ya Sabuni ikabakia mdomoni au kooni! Huenda ikasababisha kichefu chefu.

Sioni sababu ya kuosha kwa sabuni, tumia maji ya kawaida tu kuliosha vizuri. Ama kama kuna ulazima wa kufanya hivyo, tumia sabuni ya mche wa Jamaa isioacha harufu. Epuka sabuni ya Unga na sabuni za mikono yaani Hand Wash Soap.
Si anaosha ndo anamenya.
 
Back
Top Bottom