Kuongelea udaku kuna faida kubwa kuliko kuongelea maendeleo

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
13,207
2,000
1. Ukiongelea mambo ya maendeleo viongozi hawarespond na wanajidai hawasikii. Watu wamezungumza kuhusu wazo baya la kujenga uwanja wa chato hakuna aliyesikiliza. Watu wamezungumza kuhusu mradi mbovu wa daraja la Coco-Agakhan hakuna aliyesikiliza. Watu wamepiga kelele kuhusu umuhimu wa kujenga irrigation schemes hakuna anayechukulia kwa uzito. Jambo kubwa kama katiba wamelifunga na zamani tulipata ya kujadili toka bungeni lakini leo tunatoa kwenye Tv za youtube.

2. Viongozi wanafanya na wanarespond haraka sana kwenye mambo ya udaku. viongozi nao wamecheza ngoma ya cheti, wanapenda SHILAWADU, wanafanya tuwe watu wa kufuatilia nani kateuliwa nani katenguliwa, hao maRC na maDC nafasi haitatosha kuzungumzia vituko wanavyofanya.

Kwenye saikolojia kuna ishu ya behaviour na rewards. Tabia zinazokuwa rewarded ndiyo zinazondelezwa. Udaku umekuwa rewarded kuliko mambo ya maana.
 

jambo leo

Senior Member
Mar 10, 2017
144
250
Rais mwenyewee anapendaa udakuu wa mjinii ndioo maana ijumaa mapemaa tu atasitishaa hataa kazii alizonazoo akaanzee kugombaniaa rimotii na watoto wakee kisaa shilawaduu..akafiee mbelee
 

MBIIRWA

JF-Expert Member
May 24, 2013
2,491
2,000
RAIS wa zamani wa INDIA, Dr. AbdulKalam, alipata KUSIMULIA:

"Siku moja usiku, nilipokuwa mtoto, nakumbuka kumwona MAMA yangu akituletea chakuka mezani nikiwa na BABA.
MAMA aliniwekea sahani ya CHAPATI, huku akimwekea BABA sahani yenye chapati ILIYOUNGUA.

Nilijaribu kumuangalia BABA ili kuona ATAFANYAJE. Baba alianza kula CHAPATI ile iliyoungua huku akiniuliza kuhusu maendeleo yangu shuleni.

Sikumbuki nilichomjibu, ninachokumbuka ni kumsikia MAMA akimtaka RADHI baba kwa KUUNGUZA chapati. Na kamwe sitasahau majibu ya BABA pale alipomjibu MAMA kwa kumwambia, 'Oh, usijali MKE WANGU. Huwa NAPENDA pia chapati za KUUNGUA.'

Baadaye , nilipokwenda kwa baba na kumtakia usiku mwema, ndipo nilipomuuliza kama ni kweli hupendelea chapati za kuungua.

Alanza kuniambia, 'Leo, MAMA yako alitingwa mno na MAJUKUMU ya kazini hata akawa amechoka sana, ndipo akaunguza chapati. Lakini, kwa bahati, chapati ILIYOUNGUA haiwezi KUMUUMIZA mtu kiasi cha KUMCHOMA MOYONI, walakini MANENO makali yanaweza KUMUUMIZA. Hivyo, sikuwa na sababu ya KUMSHUTUMU kwa MANENO makali. Hata kama sipendi chapati za kuungua, ila kumjibu vile kumemfanya awe huru. Unajua MAISHA nayo hayako KAMILI kama TUSIVYO kamili SISI wanaadamu. Kwahivyo, ili kudumisha FURAHA na kuboresha MAHUSIANO na MAELEWANO baina YETU, ni lazima TUJIFUNZE kuyakubali na kuyakabili MAPUNGUFU yetu - Chapati za kuungua hazidumu milele, zikishasagika tumboni utakwenda kuzitoa msalani. Lakini, MANENO makali huacha majeraha ya kudumu MOYONI...

Tafakarini Wakuu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom