Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 766
- 1,884
Kwa maoni yangu, Kama kuna hasara nyingine kubwa CHADEMA wamepata baada ya kuondoka Dr. Slaa basi ni hii ya Waitara kuondoka. Ni hasara kubwa kwa Chama.
Waitara ni mwanasiasa kweli kweli. Nimefanya nae kazi zaidi ya miaka 8 na alikuwa rafiki yangu na nilikuwa napenda kazi zake hasa tulipokuwa kwenye chaguzi ndogo Igunga na Arumeru na Chalinze n.k
Waitara alipaswa kupewa nafasi aliyo nayo John Mrema au Reginald Munisi kwa sasa. Ila hofu ya Mwenyekiti wetu Mbowe ndio ilikuwa kikwazo kwake.
Huwezi kumlinganisha Waitara na Mrema au Munisi hata kwa sentimeta ila ndio hivyo hofu ikishaingia basi mambo ndio hivyo tena.
Waitara amekuwa na wakati mgumu sana Chadema tangu alipogombea Ubunge kule Tarime 2010. Mbowe alimtaka John Heche kijana wake. Waitara alimshinda Heche kwenye kura za maoni kwa mbali sana. Tangu wakati huo Waitara hajawahi kuwa na amani ndani ya CHADEMA.
Majaribio kadhaa ya kumfukuza uanaChama yalifanyika bila mafanikio. Mimi ni miongoni mwa watu waliomshauri Waitara kugombea Ukonga baada ya kuona vita imekuwa kubwa Tarime na ikisimamiwa na Mwenyekiti Mbowe mwenyewe.
Isingekuwa Ubunge Waitara angeshatimuliwa Makao Makuu nae siku nyingi pamoja na sisi. Ukweli ni kwamba sisi ni wapinzani wa Mbowe wa ndani ya Chama siku nyingi.
Mbowe ukimpinga tu Chuki ni ya milele. Visasi. Chadema itapoteza wengi kwa Chuki, Visasi na Majungu.