Kuombwa hela (mizinga) ya wakwe imenichosha

Kuombwa hela (mizinga) ya wakwe imenichosha

ulivojitambulisha kuwa bakhresa baba yako ila hutaki watu wajue ulidhani matokeo yake nini?
ulivoenda na msururu wa magari ya kuazima kuna siku ulisema umeazima?
 
Ndo mana mnaambiwa kabla ya kuoa chunguzeni kama bdo upande wa wakwe zako kuna independent
people na background yao
By the way pole ila sasa jipange kuwekeza uweze kumudu mizinga

ulitaka kumaanisha dependent

Inaonekana hujui maana ya ndoa, ulidhani ukimchukua mkeo ndio umemaliza eeh! pole mwaya. ndoa ni kuunganisha koo mbili yaani ndugu zake na ndugu zako. baba yake ni kama baba yako .

hivyo wanapokuwa na shida siyo busara kutokuwasaidia eti hujaoa ukoo mzima. cha msingi angalieni jinsi ya kuwasaidia wazazi au mpe mkeo shughuli ya kufanya ali aweze kuwapiga tafu wazazi wake.

ndiyo nyie mnauliza ooh pesa ya mwanamke inaenda wapi? ndiyo huko sasa.
kama mkeo umemfungia ndani watunze wazazi wake hakuna namna.
 
Kusaidia ni kuzuri kama unao uwezo. Ila familia yako inapopata shida kisa misaada hili ni tatizo mkuu.

Kila mwezi wanaomba? Basi watakuwa hawana aibu. Kuomba omba ni aibu aseeh. Tena kwa mkwe! ! Jitoe aibu kama walivyojitoa waeleze ukweli la sivyo familia yako haitasonga.....
 
Kama huna wambie hauna. Au uwe unawapa kidogo kidogo... Au kama vipi watafuties kitega uchumi wajitegemee. Pole sana kwa majukumu ya ziada...
 
MFUNGULIE MKEO BIASHARA TENA WASHILIKISHE NA WAKWE ZAKO KWAMBA NI KWAAJILI YENU IWE INA WAPIGA TAFF

UKIFANYA HIVYO WAKWE WENYEWE WATAONA AIBU

INAONEKANA MKEO NI BINTI PEKEE KATIKA FAMILIA YAO
 
Inaonekana hujui maana ya ndoa, ulidhani ukimchukua mkeo ndio umemaliza eeh! pole mwaya. ndoa ni kuunganisha koo mbili yaani ndugu zake na ndugu zako. baba yake ni kama baba yako .

hivyo wanapokuwa na shida siyo busara kutokuwasaidia eti hujaoa ukoo mzima. cha msingi angalieni jinsi ya kuwasaidia wazazi au mpe mkeo shughuli ya kufanya ali aweze kuwapiga tafu wazazi wake.

ndiyo nyie mnauliza ooh pesa ya mwanamke inaenda wapi? ndiyo huko sasa.
kama mkeo umemfungia ndani watunze wazazi wake hakuna namna.

Kuna wakwe wengine ni too much. Unaweza kuta mkwe anakuomba pesa za kusafiri kwenda kuwasalimu ndugu zake ama kwenye sherehe kijijini.
 
Wakwe weng ndo walivyo ukishaoa tu wanageuka omba omba kwa mkwe, waambie cna full stop wala hawata kushtak!!!
 
Wakuu,

Mimi ni mgeni kwenye ndoa, nina kama mwaka mmoja hivi tokea nimuoe mke wangu. Lakini kitu kilichonifanya niandike huu ni kutokana na kuchoshwa na kuombwa obwa hela na ndugu wa mke wangu.

Sijui utambiwa tusaidie hela ya kitu gani. Jamani matatizo hayaishi ukweni na huku mahari nilitoa na waliniganda sana wakati wa kuitoa.

Sijui nyie wakuu mliokaa kwenye ndoa kwa wakati mrefu mnaepuka vipi hii karaha.

Na hayo maombi ya pesa yanapitia wapi.? Je wanakwambia wewe direct ama wanamwambia mtoto wao/mkeo kisha mkeo ndo anakwambia.?
 
wazazi wako na nduguzo unawasaidia????........jiongeze mkuu....
 
Hao ndg wa mkeo kiboko mbona wengne hatuwasumbui hvyo waume zetu
 
Kipato chako ni kikubwa sana kiasi cha kuweza kuimudu hiyo mizinga?

Kama upo hoi financially, fanya hivi: Andaeni bajeti yenu wewe na mkeo. Weka kila kitu kwenye bajeti na maliza hela yote (as per your monthly income). Siku wakiomba tena acha mkeo ndo adeal nao maana anajua situation ipoje.

Ila kama upo njema wape tafu tu jomba...weka heshima ukweni.
Ushaur mzur sana, mshirikishe mkeo kama unakaakiba chako cha matumiz ya mwanaume mkeo asijue, sukumia mizigo yote kwake, uwenda na yeye huwa anawaambia wakuombe,
 
Back
Top Bottom