Kuomba msaada kwa Rais Magufuli kwamtoa jasho Shilole

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Msanii wa bongo fleva na mjasiriamali nchini, Zuwena Mohamed maarufu kama Shishi Baby amefunguka na kudai yeye sio mtu wa kufake maisha kama baadhi ya watu wanavyomfikiria mitandaoni huku akiwaomba radhi kwa wale ambao wamekwazika kwa yeye kuomba msaada kutoka kwa Rais Magufuli

Rais Magufuli akiwa na Shilole upande wa kulia
Shilole ametoa ufafanuzi huo leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa kijamii baada ya kuenea 'video clip' iliyokuwa ikimuonyesha akiongea lugha ya ughaibuni 'kiingereza', akimualika Rais Dkt. John Magufuli kuhudhuria katika mgahawa wake ili kusudi aweze kuonja mapishi yake pamoja na kuomba msaada wa watoto wake katika kupata elimu bora.

"Niombe radhi kwa mlionielewa tofauti mimi huwa si-fake maisha naishi maisha yangu, sina utajiri huo kama mlivyonisema hata nyumba niliwaambia nimejenga kwa kujiwekea kidogo kidogo kama mama ntilie na mwanamuziki, ndio maana nilipofikia hatua fulani nikaona ni vizuri ku-share na nyie ili muone nguvu ya 'support' yenu inavyonipa maendeleo",ameandika Shilole.

Pamoja na hayo, Shilole ameendelea kwa kusema "nilichokiomba juzi kwa baba Magufuli ni 'support' na ufadhili wa wanangu kuendelezwa katika vipaji na taaluma wanazopenda kusoma. Mimi napambana sana kuwasomesha lakini pia natamani wapate kitu zaidi ya nachoweza kuwapatia, hivyo nikaona ni kwanini nisiweke kilio changu kwa Mheshimiwa kwasababu elimu kwa watoto wa kike ni moja ya mambo ambayo naamini anayasimamia vema".

Mbali na kauli hizo, Shilole ni miongoni mwa wasanii wa kike nchini wanaopambana usiku na mchana, katika kuhakikisha anajipatia riziki kupitia maarifa aliyokuwa nayo na nguvu zake na kumfanya awe tofauti na wanawake wengine ambao wamekuwa wakisubiria pesa za mahitaji kutoka kwa wanaume zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpuuzi huyo anaomba msaada kama anauwezo wa kujenga nyumba na kugharamia gari lake na maisha yake anashindwa nii kuwekeza milioni moja kwa mwaka kwa ajili ya mwanae?kuna watu wamezaliwa omba omba natural hata Mungu awabariki vipi hawaridhiki

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu, kuombaomba ni asili ya mtu hata akiwa na uwezo bado atakua na hiyo tabia. Na watu wenye tabia hii wengi huwa wanaasili ya uchoyo na ubinafsi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pesa za kuviweka ndani vitoto vidogo.vya kiume wanazo ila ada hawana..analeta maigizo huyo mama
 
Back
Top Bottom