Unaona sasa? Kwa hiyo unatangaza kushindana na mwanaume?
ahahhhahahhaah mi kweli bana nimeolewa nchi za kaskazini lakini failure yoyote niliyopata kwenye ndoa yangu sijwahai kuona connection na makabila yetu!Tupate uzoefu wa walioolewa nchi za magharibi.
Natalia, Muke Ya Muzungu, Kongosho na snowhite (yule bf wako wa praimare muhindi)
hebu tupeni uzoefu wenu?
ndio ukweli mkuu lakini unauma!
Kaka, you have a huge world view! Big up
Wiyelele, mi nakubaliana na wewe kabisa. Kuna mambo mengi ambayo yanatofautiana iwapo mtu umechanganya haya mambo!
hata mie naunga mkono yako mengi na walio katika hali hii watakuwa mashahidi. sio lugha tu, hata shughuli nyinginezo katika maisha ya kawaida sana. tuwashauri vijana waoe nyumbani. wachagga wanasema" usioe chasaka"yaani mtu/mwanamke asie wa nyumbani kwake, nadhani waliliona hilo mapema,
Love has no boundaries!Ndugu wana JF,
Asalaam aleikum. Mmezoea kuniita mwenye matatizo lakini leo nimekuja na wazo hapa. Mi naona ndoa za wale ambao waliolea kwao au mke na mme wanatoka Mkoa mmoja naona wana raha zaidi kuliko sisi tuliooa makabila mengine haya. Kuna wakati ambapo ungapenda kuongea kilugha, lakini unashindwa. Mfano, mimi akija mdogo wangu nikiongea nae kilugha naona mke anakuja juu nakusema tuongee kiswahili. Utamu wa hadithi ni lugha, na lugha yenyewe ni ile ya mama na sio ya mke. Hili halihusiani na ukabila lahasha kwa maana upendo hauna ukabila wala dini. Lakini nahisi wenzetu wanaoongea lugha moja ndoa zao zinadumu zaidi na upendo unakuwa bomba kila wakati. Wewe unaonaje na mme wako au mke?
Of course, you will not know the boundaries if u have not experienced any problem.
love has no boundaries!
Tokoliyako
Sio kwamba natapatapa, ila naona wenzangu wana furaha sana na ndoa zao. Nilipochunguza nikaona wengi wameoa kwao au mikoa ya jirani ambayo wanaelewana lugha.
kuna raha yake lakini kazi ipo kwetu sisi ambao baba mkinga na mama msambaa.sasa hapo hata ukioa mkinga au msamba bado haina maana ya kabila moja.labda utafute mchanganyiko kama wako.
Ni kweli kabisa, saa myingine unatamani hata umpe kaumbea unashindwa kiswahili kila mtu anajua kingereza ndio usiseme lol kweli kuna raha yake.
Kwani baba akiwa Mkinga na mama msambaa, ukiulizwa kenu wapi unajibuje?