Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?
Upo huo uwezekano MMKJJ lakini kwa hali fulani tu.
Nimeona kwa mfano mwanaume ambaye amefiwa au kuachana na mkewe akataka kuoa tena ili apate mwenza ( companion) na siyo mama wa watoto.Wapo wanawake wenye kutamani kuwa na companion kwa vile labda walishazaa na hawataki watoto tena.Mara nyingi mwanaume mwenye mwanamke kama huyo, hataacha "kutafuta mtoto kando".Kwa vijana wenye umri wa kuzaa sijui kama hili linawezekana.
Kwa kifupi nadhani ulazima wa kuzaa uko kwa wanaume zaidi Nionavyo mimi.
CPU.. sasa kama mmoja wao baada ya ndoa ikagundulika au ikatokea sababu ya kutokuweza kuzaa ina maana yule mwingine ana haki ya kuzaa nje ya ndoa au ndoa ivunjike hata kama bado wanapendana?
Swala la kuzaa baada ya kuoana ni tarajio la kijamii kufuatana na tamaduni nyingi hasa za kiafrika na hata kiasia.
Wengi kabla ya kuoana hawafanyi mjadala kuona kama wakishindwa kuzaa itakuwa vipi.Matokeo yake siku hizi watu wanapeana mimba kabla ya ndoa ili kuepuka lawama huko mbeleni.
Swali la kutaka kuona kama inawezekana watu wakaoana bila kuweka matarajio ya kuzaa katika mila, desturi na tamaduni zetu, ni muhimu hasa kwa kipindi au zama hizi. Watu wanaoana kwa gharama kubwa sana, wanataka kuzaa kwa udi na uvumba lakini kibaya zaid ndoa hazidumu, watu wanaachana, watoto wanajikuta kwenye familia zilizovunjika.
Je isingekuwa bora watu wakaangalia upya umuhimu wa kuzaa kulinganisha na ugumu wa kuvumilia machungu ya ndoa kwa ajili ya kulinda haki na maslahi ya watoto wanaowataka?
Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?
Kuzaa na kulea ni MAJUKUMU ambayo kila binadamu aliyekamili anapaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa maandiko. "Mungu alipowafukuza Adam na Eva kutoka kule bustani ya Aden, aliwaambia kuwa nendeni mkazaane muijaze dunia"
Kimaisha ni suala zuri sana tena sana kupanga kutozaa kama uwezo wa kulea utakukwamisha, au hamtaweza kuvumilia machungu ya kulea watoto, lakini utajikuta unabanwa na maandiko matakatifu. Hebu imagine waliotuzaa nao wangepanga wasizae tungekuwepo hapa JF kuchangia hii mada?? Je hatuoni kama kutozaa kwa makusudi ni dhambi kwa maana ya kuzuia kusiwepo vizazi vijavyo???
Tujadili . . . .
Mzee Mwanakijiji, kuoa ni wajibu ila watoto ni majaliwa.Kwamba watu wawili mnaopendana mnaamua kuoana na kuishi maisha ya pamoja bila kutaka kuwa na watoto au kupanga kuwa na watoto. Je hili linawezekana katika jamii yetu au kila ndoa inapimwa kwa mafanikio ya kuwa na watoto na kwamba bila ya watoto ndoa inaonekana kama haikamiliki na hivyo mtu yuko radhi kufanya "lolote" ili awe na watoto?
Ndugu zangu hawatakawia kuniwekea vikao kuwa kwanini sishiki mimba.
Mi nataka watoto, nikitaka mwanaume wa kustarehe naye wapo wengi tu, kuanzia makuli hadi maofisa