Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

Kuoa mwanamke mwenye mtoto ni shida

emma shayo

Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
78
Reaction score
16
Mimi ni kijana na 28 years nilikutana na binti nilimpenda sana kumbe alikua na mtoto kazaa na mwanaume mwingine na mimi pia nilikua na mtoto wa nje niliona isiwe sababu nikaamua kuishi nae toka 2013.

Nilimkuta akitumia sindano za uzazi wa mpango nikamsihi aache akaacha mpaka leo hajawah pata mimba ilileta ugomvi mpaka ikafikia kuniambia mtoto niliezaa na mwanamke mwingine nimesingiziwa iliniuma sana ila nilihamia Mbeya kikazi niliamua kumsaliti nikaanza mahusiano na msichana mmoja akabeba mimba akajifungua mtoto wa kike.

Imeendelea nikaamua kumwambia ilikua ni mziki tuliendelea tukaenda hospital akaangaliwa docta akasema mirija ya uzazi imeziba nilitumia gharama kweli amepona ila mimba bado sasa mimi mtoto wangu wa kwanza yupo std 1 hatujawahi ishi nae yupo kwa wazazi wake na wake yupo kwa wazazi wake.

Imeibuka leo anataka kumleta mtoto aishi na mimi wakati mimi sipo tayari jamani imekua ni ugomvi anaforce kumleta, kiukweli mimi sipo tayari, kaniambia bora tuachane kuliko asiishi na mwanae.

Naombeni ushauri jamani nifanyeje maana kwanza nimechoka kabisa ushauri pliz
 
Mkuu ni ngumu kwa mwanamke kuishi mbali na mtoto wake,hilo inabidi ukubaliae nalo,lkn pia naona kama huyo dada umemtamani aua unajilazimisha,ungekuwa umemependa usingeona taabu kuishi na mtoto wake,sikiliza moyo wako vuzuri
 
Kwaiyo kama wewe humthamini mwanao unataka naye akuige?,kwani huyo mtoto atapunguza nini?
 
Mwache amlete tu mwenyezmungu atakuongezeq rizk na kukupa moyo wa subra nawe ikiwezekana mlete na wako walelewe pamoja
 
Kuoa mwanamke mwenye mtoto kuna changamoto mkuu, hapo bado hazijaanza story za kuonana na baba wa mtoto sijui na mambo gani mengine. Unatakiwa kua na moyo mgumu ila kama unampenda sikiliza moyo wako unasemaje,jambo la kuishi na mwanae mkae mzungumze isiwe anataka kukuendesha,uwe na msimamo na uonekane kusimamia unachokisema. Usiogope kufanya maamuzi magumu pale utakapoona ujinga.
 
Hatukuwa na makubaliano yoyote

Mkuu ni ngumu kwa mwanamke kuishi mbali na mtoto wake,hilo inabidi ukubaliae nalo,lkn pia naona kama huyo dada umemtamani aua unajilazimisha,ungekuwa umemependa usingeona taabu kuishi na mtoto wake,sikiliza moyo wako vuzuri
 
Mkuu ni ngumu kwa mwanamke kuishi mbali na mtoto wake,hilo inabidi ukubaliae nalo,lkn pia naona kama huyo dada umemtamani aua unajilazimisha,ungekuwa umemependa usingeona taabu kuishi na mtoto wake,sikiliza moyo wako vuzuri

Daaa inauma lakn maana upande wa ndugu zangu najua wataongea sana
 
ukipenda boga penda na maua yake wanaume sijui tuna tatizo gani kwenye hili sasa unampenda mwanamke mtoto wake humtaki kweli? afu in future utajikuta na wewe unataka uishi na mtoto wako huyo wa demu mwengine afu utataka kumforce huyu dada akubali na kwa upendo anaweza akakubali sijui hii dhambi ya ubaguzi utatubu au?
Yani binadamu kumbagua binadamu mwenzie hii dhambi ni sawa na kula nyama ya mtu
 
Mwache amlete tu mwenyezmungu atakuongezeq rizk na kukupa moyo wa subra nawe ikiwezekana mlete na wako walelewe pamoja

Mm pia inaniuma kuishi mbal na mwanangu but wazaz wangu kumwachia dogo inakua ngum sana wanadhan mtoto kuishi na mama wa kambo atanyanyaswa
 
Mpende huyo mtoto huwezi jua kesho wewe humpendi huyo mwanamke ungempenda usingetaka akae mbali na mwanae mbona wako anakaa na mama yake.
 
Daaa inauma lakn maana upande wa ndugu zangu najua wataongea sana
ukimpenda kwa dhati hicho hakitakuwa kikwazo....yaani ukimpenda hata ukiambiwa amezingirwa na moto utaingia kumuokoa,narudia tena,tafakari vizuro ,huenda umemtamani
 
Daaa inauma lakn maana upande wa ndugu zangu najua wataongea sana
dont live to please someone acha kufurahisha nafsi za watu wengine hata pale ambapo wewe unaumia ndugu wataongea hutaki waongee binadamu kapewa mdomo kwaajili ya kuongea na kupitishia chakula kuongea ni moja ya sifa ya ukamilifu wa mwanadamu wataongea but finally itakuwa ni wewe na maisha yako na huyo mwanamke thats all ukitaka kumfurahisha kila binadamu hapa duniani hakika utakufa sababu wapo ambao watafurahi sana kuona ukiumwa au ukisota na maisha magumu je upo tayari kuwafurahisha au kuogopa maneno yao
 
Best ni bora mkawachukua watt wenu wote mkaishi nao pamoja, hapo kwa pamoja watajenga mahusiano mzur ambayo ni hazina hata kwa badae... Kwanza watt hao ni wenu sio WA hao mlio watelekezea, kuwa na busara Mr.
 
Kuoa mwanamke mwenye mtoto kuna changamoto mkuu, hapo bado hazijaanza story za kuonana na baba wa mtoto sijui na mambo gani mengine. Unatakiwa kua na moyo mgumu ila kama unampenda sikiliza moyo wako unasemaje,jambo la kuishi na mwanae mkae mzungumze isiwe anataka kukuendesha,uwe na msimamo na uonekane kusimamia unachokisema. Usiogope kufanya maamuzi magumu pale utakapoona ujinga.

kwangu iko hivi mkuu..
Mimi bana nimekukuta na mtoto unalea pekeako,nimekupenda nikakubeba na mwanao,ukishafika kwangu sitaki tena uniletee habari za baba wa mtoto wala nini,kama anamtaka mwanae mpelekee ww urudi hapa kama wewe na wewe huwezi kuishi bila mwanao nenda usirudi.Sitaki kabisa habari ya kuniambia naenda kumsalimia baba wa mtoto stupid wakati nilikukuta pekeako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom