Mke amefungua pub bila kunishirikisha na anauza mwenyewe kama bar maid nyumba imewaka moto Sababu mke amekua jeuri na kiburi,so aggressive hakuna unachouliza ukajibiwa kistaarabu. Kila mteja anayeenda pale akiomba namba anapewa tu bila shida yupo bize muda wote ni pub pub na `wateja wake" kama anavyowaita hajali familia wala ndoa tena nyumba,chumba chakulala kimekua km stoo kitanda ndio usiseme hajali na imefikia hatua naambiwa nisifike hata kwenye biashara yake sababu namfukuzia wateja wake.
Tupo kwenye ndoa yakikatoliki mwaka wa 4 sasa na tuna watoto wawili wadogo 4yrs na 2yrs.
Ushauri, nifanye nini?