Kuoa mke ANAYEKUZIDI Umri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuoa mke ANAYEKUZIDI Umri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eng. Y. Bihagaze, Sep 21, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  MKE ANAYEKUZIDI UMRI

  Kwa kuwa mimi ni Mkristo labda nianze Kwa ku-quote maneno ya biblia Kwenye kitabu cha Mithali 24:27 inasomeka ''Tengeneza kazi yako huko nje, Jifanyizie kazi yako tayari shambani, Ukiisha, jenga nyumba '' Huwezi Kuijenga Future yako imara kabla ya Kuijenga Nyumba yako kwanza Yaani wewe Na Mke wako.. Umapema wa kujenga Ndoa ndio umapema Wa Kuunda strong future..

  Katika maisha haya uhadaa mkubwa wa DUNIA Ni kumkamata Mtu Na Nyumba yake.. Mume ni nafasi ya Roho Na Mke mwili Na maisha ni nafsi hai...

  Pia Katika maisha haya chini ya jua nimegundua Jambo la ajabu sana.. Kuoa Mke anayekuzidi umri kuna utukufu wa ajabu sana.. Nimeshangazwa baada ya kugundua kwamba watu mashuhuri sana hapa duniani walioa wake waliowazidi umri.. Nitaje baadhi Yao watatu tu ili maada isiwe ndefu

  1. Mao Zedong maarufu Kama Mao Tse Tung mnazi mkubwa kabisa siasa Za kikomunist, alikuwa kiongozi Wa vuguvugu la mapinduzi CHINA. Ndiye mwanzilishi Wa Jamhuri ya watu wa China.. Ndugu huyu aliyezaliwa 1893, alioa mwaka 1901 akiwa Na miaka Nane , alimwaoa bi Luo Yixiu aliyekuwa na miaka 13 aliyezaliwa 1889. Ingawa baadae mkewe alifariki akaoa Mwingine ..

  2. Mohandas Karamchand Gandhi maarufu Kama Mahatma Gandhi, kiongozi wa taifa la India aliyeongoza mapinduzi wakati India ikitawaliwa Na mwingereza.. Alizaliwa 1869, akiwa Na miaka 13 tu alimwoa Kasturbai Makhanji aliyekuwa Na miaka 14..

  3. Tuje Marekani , mwanzilishi Wa Taifa Hilo mashuhuri , George Washington aliyezaliwa February 1732, alimwoa Martha ambaye alizaliwa June 1731.. Walioana Kwenye miaka ya 27..

  Kwa haraka utaona ndoa hizo Za utotoni ziliwajenga zaidi kinyumba Na baadae wakatengeneza future.. Gandhi aliyeoa ana miaka 13, mkewe 14, waliishi maisha ya NDOA miaka 61, Gandhi akafa akiwa Na miaka 74 mkewe 78.. Mimi Kwa hoja chache naweza jenga faida Kama 11 Za Kuoa Mke anayekuzidi umri bila hasara..

  1: Anajiheshimu, anajiona ni mkubwa so inshu Za upuuzi hazipi nafasi.

  2: Anamtii sana mumewe Kwa sababu asipomtii sana mumewe Basi ni rahisi Mume kuhisi anamdharau Kwa kuwa Na Mdogo .. Na Utii ndio tunu pekee ndani ya NDOA.

  3: hawezi kumfokea au kumgombeza mumewe Kwa sababu nature ya umri..

  4: hujiona tu ana wajibu mpana sana ndani ya familia, hakurupuki

  5: ni rahisi sana kusamehe, makosa ya Mume huyachukulia kama makosa ya mdogo wake..

  6: Mume huwa mwangalifu sana Kwenye kuijenga nyumba yake, hakurupuki Kwa sababu atachelea Kufanya utoto Na mkewe kumcheka ..

  7: wakati Wa mashauriano Wanashauriana kila Mtu akiwa Kwenye Enzi yake, Mume akishikilia Kama Kichwa Cha Nyumba huku akitambua anayenishauri kaliona jua kabla yake..lazima awe makini sana

  8: Mke humstahi sana Mume wake, hamropokei nje, hujihisi atabezwa kwanini ameolewa Na mdogo so hustahi mambo mengi..

  9: Mke hujiona ana nafasi ya kuyajenga maisha ya familia zaidi kuliko kutapanya Mali

  10: Mume humwona mkewe mkubwa mwenzake Na humwachia baadhi ya majukumu Kwenye familia ayaendeshe yeye akiwa mbali bila kuhofia kwamba Mke anaweza vurunda

  11: HAWANYIMANI..
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mmmh mmi kutembea na mdogo wangu siwezi jamani...si ni kumbemenda huko?
  mbona wazee kibao
  mimi sishauri kabisa wanawake kuolewa na wadogo zetu
  sasa utavuaje nguo?
  hapana aise! hainogi hata
   
 3. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  ngoja wenye aina hizo za ndoa wachangie, hubby wangu mie kanizidi miaka kadhaa, sasa nikisema hapa nitakuwa mmbeya!
   
 4. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mwishoni yanitokee haya !akuuu![​IMG]
   
 5. by default

  by default JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada vipi we ushamuowa dada yako nini? Miaka 13 na 14 washaowana hapo nafikiri serikali zilikuwa zimelala bongo lazma mkanyee ndoo .mi cwezi hata kucheat na aged kwangu aise
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Eng. Y. Bihagaze Atakapo kuzeekea wakati kwanza wewe ndio unachanua ndio utaonja tamu ya chungu.
   
 7. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Luckymito...Kwahiyo sisi wanaume tukivulia wadogo zetu nguo ni sawa?
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Adamu na Eva nani aliumbwa kwanza?
  tuache nature ifate mkondo wake
   
 9. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyo mwanaume atakuwa hana kauli ndani ya nyumba.
   
 10. salito

  salito JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Ntarudi badae
   
 11. g

  gurumeti Member

  #11
  Sep 21, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  katika ndoa maandiko yamesema;wake watiini waume zenu, waume wapendeni wake zenu. maandiko yameenda mbali na kusema waume ishini kwa akili na wake zenu. Age is just a numbers in marriage but gape isiwe kubwa mno! wewe binti ukiolewa na mzee anayekuzidi more than 7 years hujitendei haki kadhalika na kijana!
  Faida zilizopo hapo juu ni zaidi ya hapo, zingine hizi hapa;

  12. mume hachoki kumfikisha kileleni mke wake muda wote na wakati wote
  13. mke hufurahia sana tendo la ndoa kutokana na faida na. 2, 4, 8 na 13
  14. mume huchukua nafasi yake(kichwa) ktk nyumba kwelikweli
  15. maisha(maendeleo) yanakwenda fasta, bcoz kuna ushirikishwaji. mume hakurupuki..., mke hakurupuki wote wapo makini kama mtoa madaalivyoeleza.
  16.RAHA TUPU.....!

  NOTE:
  watu wengi hufikiri hili ni tatizo kwa sababu;
  1. upande wa mume
  -waume wengi hukurupuka ktk maamuzi ya familia
  -waume wengi hawawatii wake zao, huona ngumu kuomba radhi wanapokosea.
  -waume wengi hupuuzia ushauri wa wake zao kwani huona hawajui kitu(hasa binti unapojikabidhi kwa pejedee ukidhani kuwa umepata kumbe umepatikana)
  -etc
  2. upande wa mke
  -wake wengi hawataki kufanya kazi, huhitaji cheap life!
  -wake wengi huhitaji "ready made" kitu ambacho ni hatari sana.
  -wake wengi hawawatii waume zao.
  -wake ambao wameolewa na wazee/pejedee baada ya muda hutamani sana vijana wenzao!
  -etc

  JF wenzangu, kuna siri kubwa ukioa anayekuzidi. siwashauri naeleza kile nachokifahamu!
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  km anakimilik vyema kitanda
  analeta mkate mezan
  ana busara na hekima
  anajua wu is he n mimi ni nan kwake then ahhh gooooooooooooooooooooooddd to go....cha msing nipo happy nae no bfu wala inferiority cmplx....WAWEZA OWANA na lijitu likubwa lakin likawa zaid ya mtoto....BEHAVIOR N UNDESTANDNG IS OL NIDED.


  mabata madogo dogo oyeeeeeeeeeeeeeeee.......!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  shosti mzima .......mkipishana sana hainogi ipo siku atakuona umezeeka atakwenda kuogelea na mabata wadogo wadogo
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Raha mwanamme awe mkubwa kwa kweli
  Hivi unaanzaje kideka kwa kindagateni???

  Si bora udeke kwa fao la uzeeni lol
   
 15. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nimependa kwamba huyo dada hatashtakiwa ambayo ni fair kabisa. ingekuwa bongo angeenda kumpa kampani lulu miaka kadhaa wakati "uchunguzi unaendelea".

  EDIT: wtf!! hiyo habari ni tarehe 01/04, sio utani wa siku ya wajinga?? Luckymito hiyo source nina mashaka nayo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hivi akienda kucheza na watoto wenzake utalaumu?
  Watoto wana haki ya kucheza! Lazima haki za mtoto zifatwe jamani
   
 17. i

  issabela Senior Member

  #17
  Sep 21, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ilinitokea nishawah kudate na boy nlomzidi miaka miwili na miezi kadhaa thou tulipendana sana lakin nilikua najiskia aibu kwa kweli wala sikuwa na uhuru wowote ule nilishukuru 2lipobreak up hapana kweli bora kuolewa na aliyekuzid umri
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  He he he, unawaza kujenda baba mwenye nyumba analilia game ya Ben 10.

   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  teh teh ukiangakia bbc news analilia movie ya kirikuu
   
Loading...