Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Moja kati ya maadui wakubwa wa usingizi ni mdudu ‘kunguni’ ambaye anaweza kumfanya mtu anayepanga kujipumzisha kuhisi anaadhibiwa kwa kufinywa.
Usiku nikiwa nimelala nahisi kuna vitu vinang'ata na kutimua mbio, naendelea kulala hali inajirudia sana nahisi ni mbu tu, Nimeamka Asubuhi Naangalia Utando wa Chandarua na Kuona vitu mithili ya maua vikiranda na kuvinjari nikiangalia kwa makini nagundua io mbu kumbe ni kunguni almaarufu vi-gofu
Nauliza wenyeji asubuhi naambiwa huku kunguni wimekua kama nyumbani kwao na ni ukanda wote huu na mbaya zaidi unawakuta si Guest tu hadi kwenye mabasi hivyo huna a kuchcomokea
wenyeji wanasema kuna dawa ilipulizwa ambayo imechagiza kuongezeka kwa kunguni ukanda wote huu ingawa sijawa na hakika na hilo sana
naamua ku google BBC wansema hata Marekani Kunguni wapo na hajapatiwa dawa ya uhakika
Nawashirikisha uzi huu ili wenzangu sasa muwe makini na wadudu hawa hasa meundapo maeneo tajwa na kwingineko na jitahidi ukirudi nyumbani kila kitu mwagia maji ya moto kabla ya kuingiza ndani la sivyo na wewe utaiimba ule wimbo wa mgeni ..................
NASADIKI YOTE NILIYOYAANDIKA HAPA NA MIMI NIMERUDI NAO ...........