Kungekuwa na mikutano ya hadhara, Tundu Lissu angekiona cha mtema kuni

Kiufupi mada yako imekosa mashiko na uzito, maana umejikanganya sana.
Kwa mfano....

1/Moja ya hoja kuu ya Lissu ni kuhusu amri ya kidekteta ya Sizonje ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya Upinzani. Na mleta mada unasema kama mikutano ya kisiasa ingeruhusiwa basi Lissu angekiona cha mtema kuni! Sasa mantiki yako ni nini? Unamuunga mkono Lissu katika hoja yako hiyo au unampinga?
Hueleweki kabisa.

2/Suala lingine unasema Mikutano ya kisiasa ingeruhusiwa basi Lissu angejibiwa vizuri Kisiasa!!
Unataka kusema nini hapo?
Kama Lissu ameweza kujenga hoja zake pasipo mikutano ya jukwaa la kisiasa na kuichanganya CCM yote na Serikali yake yote, sasa nini kinashindikana sasa kwa CCM na Serikali yake kushindwa kujibu hoja za Lissu pasipo mikutano ya kisiasa?

3/Mpaka sasa CCM inafanya mikutano yake ya kisiasa nchi nzima, kuanzia mwenyekiti wake taifa mpaka wajumbe wa nyumba kumi kumi wa CCM wanafanya mikutano, na wakati huo huo wapinzani wamezuiwa kabisa. Nini kinawafanya CCM washindwe kabisa kujibu hoja za Lissu na wabakie kupayuka mashudu matupu.

4/Hoja za Lissu ni Nzito, Tamu na Ziko wazi kwa kila mtu mwenye Akili timamu. Hakuna haja ya mleta mada kuja kulalamika hapa wakati jukwaa liko wazi kwa yoyote kuja kujibu. Mleta mada ni kada mzuri wa CCM, Funguka hapa hapa Jukwaani ujibu hoja zake kama unaweza. Maana Sizonje kashindwa kuzijibu kaishia kutoa vitisho tu, Ndugai kashindwa, Pole Pole ndio kachanganyikiwa kabisa, Majaliwa ndio hata hajui hata pa kuanzia.
Huyu Petro E. Mselewa nilidhani ni msomi ila baadae nimegundua huko Mahakani anaogelea tu...either ni Gvt Lawyers make wao ndio brain zao ziko hoi

JPM KAMATA WEZI
 
CHIKIRA MTABARI=NAHUJA

Halafu mods wakakuunganishia ID

Lexus Mayai
 
Back
Top Bottom