Kunawatu wanakatisha tamaa kuhusu Katiba mpya

mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
626
Pamoja na kilio cha watanzania tuliowengi cha kutaka katiba mpya,nakadri moto huu
wa katiba mpya unavyoendelea kupambamoto kila kukicha,kuna baadhi ya watu wana
katisha tamaa wenzao kwa kupinga katiba mpya. East African radio jana walikuwa na
mada ya katiba ktk kipindichao cha super mix kinachoendeshwa na wakina Zembwela.
Cha kushangaza kila mwananchi aliyepiga simu na kutaka katiba mpya,watangazaji wa
kipindi walipinga waziwazi na wanakushambulia kwa maneno makali! eti wanadai kwa
nza tuijue na kuielewa iliyopo hata ndani ya miaka 10,kisha ndipo tuamue. Haitoshi wa
tangazaji hao wakasema labda katiba mpya ni janja ya wanasiasa [hasa wa vyama vya
upinzani kutaka kushika dola]. Swali langu kwa wakinaZembwela na watu wote wanaopinga
katiba mpya eti mpaka waijue iliyopo ni - Hivi unapoenda kupiga kura na kumchagua Raisi au
mbunge unakuwa unamjua historia ya maisha yake yote toka utotoni till ameingia kwenye
siasa? kwanini usiseme siwezi kumchagua Rais au mbunge mpaka niijue historia yake? kwa
nini ukipata kazi somewhere usiseme siwezi fanya kazi office hii till niijue history yake kuanzia
TRA,EWURA mpaka owner wa office? ACHENI UNAFIKI NYIE WATU! Ukweli ni kwamba kila
kitu kihusianacho na siasa tunafanya kwa HISIA tu na pia mjue kwamba SAUTI YA WENGI
NI SAUTI YA MUNGU! Katiba mpya ni leo na si kesho. Nawasilisha wandugu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom