Kunani ongezeko la magari yanye ngao (bullbar) barabarani, zinaruhusiwa na wengine tufunge?

Kunani ongezeko la magari yanye ngao (bullbar) barabarani, zinaruhusiwa na wengine tufunge?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
5,032
Reaction score
15,569
Kwa kumbukumbu zangu magari yenye ngao yalipigwa marufuku kwa sababu ya usalama wa watumiaji wengine wa barabara.

Hii ilisaidia kidogo madereva kuwa makini, hata kama una gari kubwa ilikuwa lazima uwe na nidhamu, ukigonga wenzako basi ujue fedha ya taa na bampa zinakuhusu.

Sasa hivi kila basi wamefunga hizo kitu, mpaka mabasi ya jeshi! Lakini wa malori nao wamenza. Pia pick up trucks hawako nyumba.

Naomba kuuliza kama zimeruhusiwa kisheria ili na sie wengine tukachomelee kwenye 'bebi woka' zetu ili tukwaruzane vizuri huko barabarani.

images (1).jpeg

images (2).jpeg
 
Back
Top Bottom