Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nassib Abdul, Maarufu kwa jina Diamond Platnum, leo ametangazwa rasmi kuwa balozi wa GSM Mall. Diamond ambaye amejinyakulia tuzo mbalimbali za hapa nyumbani na kimataifa leo ametangazwa na uongozi wa GSM Mall kuwa balozi wa Kampuni hiyo inayojihusisha na uuzaji wa bidhaa mbalimbali za majumbani. "Nawashukuru sana GSM Mall kwa kunipa ubalozi huu kwani wangeweza kutafuta msanii mwingine nje ya nchi lakini wameonyesha uzalendo mkubwa,"amesema Diamond. Hata hivyo, Diamond ameyaomba Makampuni mengine hapa Tanzania kuwatumia mabalozi kutoka hapa hapa nchini.