Kunani CHADEMA na siasa za Tanzania

Lord K

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
213
37
Kila uchaguzi tunaona chadema ikipata support kubwa sana kutoka kwa wananchi ila matokeo huja tofauti na muonekano wa kampeni zake...KUNANI HAPA?:A S 13: MI SIELEWI
 
1.Kuna mpango wa kuINGIZA MAMLUKI 5000 tokea Wilaya ya Monduli kwa Manywele!
2.Vyombo vya Usalama (Magari na Askari)vimeingizwa toka mikoa yote ya jirani, Manyara, MKilimanjaro Tanga na Dar! ...hii ni kutishia yeyote atakayethubutu kubaki kituoni baada ya kura!
 
una uhakika hao wananchi wote wanakuwa wamejiandikisha? labda wengine huwa wanauza shahada zao sababu ya kuendekeza njaa ya mda mfupi watu wanadai ccm kwa kutumia vyombo vya dola na vingine wanaiba kura,.yani pamoja na kununua shahada lakini bado kura hazitoshi hadi wanachakachua....ndivyo ninavyosikia mitaani
 
yanayofanywa na watawala ndio yanayo wasukuma wananchi wengi kuendelea kuiunga mkono chadema,pia wananchi wamechoka kuona baadhi ya viongozi wazalendo wakitishiwa kuuwawa au wakipewa sumu" wananchi wakawaida wamechoka kusubili maisha bora kwakila mtanzania nasasa wanaamini chadema ndio mkombozi wao ndio maana wako tayali hata kuchangia walichonacho kufanikisha ukombozi....Ikifika uchaguzi mkuu ujao ndio utajua namna watanzania hasa vijana watakavyojitokeza kwa wingi kuipigania chadema Ishike dola ili Iweze kulinda rasilimali za taifa hili.
 
Sababu ni kuwa CCM wanaendeleza udhalimu wao, ila chadema tunasema ALUTA KONTINUA maana yake MAPAMBANO YANAENDELEA. Kama hujui tuko vitani kumng'oa adui wa ustawi wa taifa letu (CCM) ambaye ndo donda ndugu la maendeleo ya Mtanzania, Mungu mkubwa tutashinda tu. Fuatilia Mao, Che Guevara, Fidel Castro, Samora Machel, Patrice Lumumba , Kwame Nkrumah,John Garang, n.k walipambambana na wakashinda, nakuhakikishia CCM itashindwa very soon omba Mungu wako uwe hai tu.
 
tuliyaona kwenye mikutano ya CUF miaka ya nyuma. au wewe umezaliwa mwaka gani?
Ni pemba tu ndo walioweza kujaa kwenye mikutano na wakaweza kujaa kwenye kupiga kuwa na baadae wakajaa kwenye ushindi.
 
Kila uchaguzi tunaona chadema ikipata support kubwa sana kutoka kwa wananchi ila matokeo huja tofauti na muonekano wa kampeni zake...KUNANI HAPA?:A S 13: MI SIELEWI
Watapigiwaje kura na siasa zao za majitaka?
 
Wanakuwa hawakujiandikisha kama wapiga kura.
Wanakuwa wamejiandikisha ila wapiga kura hubadili mwelekeo waonapo siasa zao za maji taka na zilizojaa sra za kisanii na hasa pale ambapo watu mbalimbali huweka bayana maovu yao kama hili linalomtafuna SLAA na matumizi mabaya ya fedha za chama. Kwa kifupi ni kwamba wananachi huchambua mbichi na mbivu dakika za mwisho.
 
Sababu ni kuwa CCM wanaendeleza udhalimu wao, ila chadema tunasema ALUTA KONTINUA maana yake MAPAMBANO YANAENDELEA. Kama hujui tuko vitani kumng'oa adui wa ustawi wa taifa letu (CCM) ambaye ndo donda ndugu la maendeleo ya Mtanzania, Mungu mkubwa tutashinda tu. Fuatilia Mao, Che Guevara, Fidel Castro, Samora Machel, Patrice Lumumba , Kwame Nkrumah,John Garang, n.k walipambambana na wakashinda, nakuhakikishia CCM itashindwa very soon omba Mungu wako uwe hai tu.

Wataishia kusema tu wanadhulumiwa mpaka pale watakapoacha kupeana vyeo kiukoo, mpaka watakapoacha kutukana majukwaani na mpaka pale watakapoacha kutumia raslimali za chama kwa ajili ya MBOWE, SLAA Na MSHUMBUZI.
 
tuliyaona kwenye mikutano ya CUF miaka ya nyuma. au wewe umezaliwa mwaka gani?
Ni pemba tu ndo walioweza kujaa kwenye mikutano na wakaweza kujaa kwenye kupiga kuwa na baadae wakajaa kwenye ushindi.

Afadhali umewaambia. Kubebwa majukwaani si kupigiwa kura. Nini kubebwa bwana Murema gari lake lilisukubwa toka Uwanja wa NDege wa JK nyerere hadi makao makuu ya Chama lakni aliishia kukiunga mkno CCM baada ya kukubali kuwa ni itabaki kuwa Chama kinachowajali watu wake.
 
CCM inatumia mbinu chafu na usalama wa 'taifa' kufifisha jitihada za wananchi kujikomboa; nikweli huwa wanaiba, lakini pia sheria ya kujiandikisha kupiga kura ni ya kifisadi, piga picha mara ya mwisho watu waliandikishwa lini kupiga kura? piga picha vitambulisho vinavyopotea, kununuliwa nk; halafu sheria inaruhusu mtu ambaye kajiandisha na shahada yake imepotea ajaza form no. 17 ili aweze kupiga kura la NEC ya CCM huwa inakataa huo utaratibu hata Meru umekataliwa, kwasababu wakifanya hivyo vitambulisho ambavyo vimenunuliwa na CCM vitatumika na wao wamenunua ili hizo kura zipigwe kwao kwa kutumia mamluki wao! Ila natoa angalizo kwa CCM mwisho wa mbinu hizi kufanya kazi umewadia, na hapa Arumeru hatuta kubali huo ufisadi, tutalinda kura kwa gharama ya risasi na mabomu wakae wakijua hivyo!
 
Wataishia kusema tu wanadhulumiwa mpaka pale watakapoacha kupeana vyeo kiukoo, mpaka watakapoacha kutukana majukwaani na mpaka pale watakapoacha kutumia raslimali za chama kwa ajili ya MBOWE, SLAA Na MSHUMBUZI.

Mwizi wewe; ufisadi mnaofanya nyie CCM ni mkubwa hata hauelezeki; acheni kuwapaka matope watu safi na watetezi wa taifa hili.
 
Back
Top Bottom