R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,138
Ni vema sana kutembelea kijijini kwenu mara kwa mara kuendeleza ukaribu na sehemu yako ya asili, likizo ya wiki mbili si mbaya mara moja kila mwaka,
Kuna wimbi kubwa kwa watu mijini hawana ukaribu kabisa na sehemu zao za asili, Unakuta mtu alipelekwa huko kijijini mara mbili tu akiwa mdogo na ndio imetoka hio, hapo kwa kawaida hakuna ukaribu wowote maana hata watu aliowakuta udogoni washapitia mabadiliko mengi.
Wengine ndio kabisa hata kwao huko hawakujui, wapo mijini tu.
Hii hali ni mbaya sana, watoto kila mwaka inabidi wazoeshwe kupajua asili yao ilipo nao waendeleze utamaduni huu kwa vizazi vijavyo visisahau asili yao.
Hii huwa inaleta hata kiu ya kupaendeleza kwenu, mnaishi mjini nyumba nzuri ila kijijini kwenu nyumba inatia aibu, hii inaleta hasira ya kutaka kupaendeleza kwenu
Mnaishi mjini sehemu nzuri ila kijijini kuna nyumba mbili tu nzuri za maprofesa ambao hawajasahau kwao, hii ni aibu, hapa mkianza utamaduni wa kurudi kwenu nyumba nzuri zitazidi.