Kuna Wenzangu waliokimbia Additional Mathematics kama mimi?

Naam, Mimi nilisoma hili somo tena kwa ushauri wa rafiki yangu pale Azania,issue ikaja mwalimu wa somo hamna pale Azania ila kwa vile tulitaka sifa basi tukasaini,
Mwl wa Tuition jamaa anaitwa Log man pale mchikichini daah nilipambana nikaenda Jitegemee kulikua na dada nae anasoma hilo somo so alinipigia mapindi, mwisho wa siku Basic Mathematics nilipata A na Additional Mathematics C,
 
Kweli,km mimi chemistry ilinitoa nock out,ila language nilikuwa vizuri,yote maisha huku uraiani tunakutana wote na maisha yanasonga
Mambo ya shule ndio ivyo hakuna mtabe wa kila kitu.. tuna connect connect mwisho wa siku tunatoka mzee
 
Ulikuwa vizuri mzee baba.. A ya mahesabu
 
Safi sana.
 
Hahaha ilikuwaje?

Mimi hili jina sijui hata maana yake limekuwa na historia tamu kwenye maisha niliyopitia
Lilikuwa la mshkaji wangu
Kuna kijiji kimoja huko mufindi kilikuwa na gari moja tuu, ( bus) na kwenda mjini ilikuwa lazima uwahi mapema sana around saa kumi ili uliwahi,msangarufu
 
Mwaka 1996 tuliletewa mtihani wa kuhitimu kidato cha nne ambao karibu section A yote ilikuwa na maswali ya additional mathematics wakati sisi hatukuwahi kufundishwa additional math. mbona tulijuta hadi mwalimu mwenyewe aliinua mikono. Wengine tulikuja kuponea kwenye section B ndo tukaambilia C wakati katika hali ya kawaida tungepandisha mabanda. Adavance nilienda PCB na sikujutia uamuzi huo kwa sababu hakuna kitu kilichonizingua kama kukaa hapo siku nzima na ku-solve mahesabu.
 
Daa heko mkuu yaani huo mwaka ndio wengine tunazaliwa
. Additional mathematics sio rahisi mtu wa basic math kutoboa maana ina chembechembe ya advanced math maana kuna hadi topic za integration, differentiation, na logic
 
Daa heko mkuu yaani huo mwaka ndio wengine tunazaliwa
. Additional mathematics sio rahisi mtu wa basic math kutoboa maana ina chembechembe ya advanced math maana kuna hadi topic za integration, differentiation, na logic
Sema ni BAM iliyo na chembe chembe za pure.
Ni A'level tupu.
 
Nimemaliza shule sec 1991 ( wengi wenu humu mlokua viunoni nikiangali cheti changu cha o level Nina F ya addition nakuficha binti yangu asikione naumia aisee
 

Nilitamani sana kufanya hilo somo O’ level. Sikupata nafasi hiyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…