Kuna Wenzangu waliokimbia Additional Mathematics kama mimi?

Nimemaliza shule sec 1991 ( wengi wenu humu mlokua viunoni nikiangali cheti changu cha o level Nina F ya addition nakuficha binti yangu asikione naumia aisee
Nina F ya CIVICS na HISTORY sinaga hama na cheti changu.. ningekiwa na uwezo ninge yarudia ku clear 😊😊😊
 
Mimi kwangu nitofauti kidogo foundation ya namba kwangu ilikua nzuri sana na niliipenda kupita maelezo. Sasa kwenye option pale form 3 nikaenda addit napo nikawa naipiga balaa. Nadhani mwishoni niliendekeza michezo Necta nikala B ya Basic na C ya addit

Advance wakanipeleka PCM nikaona shule si ndio hii michezo ikaongezeka bana, kuja kushtuka nipo form six tunajiandaa na Mock ndo pressure ikaanza nikiwaza kudifferentiate constant. Nikakomaa dakika za mwisho nikaambulia D ya Pure Math na overall nikalamba Div II 12.

Chuo nilienda zangu Biashara Bcom Accounts na hadi leo sijajutia maamuzi japo application ya namba naitumia sana na inanibeba. Ila kwenye post graduate ya Actuarial pure ilinisaidia sana pia.
 
Mimi kwangu nitofauti kidogo foundation ya namba kwangu ilikua nzuri sana na niliipenda kupita maelezo. Sasa kwenye option pale form 3 nikaenda addit napo nikawa naipiga balaa. Nadhani mwishoni niliendekeza michezo Necta nikala B ya Basic na C ya addit

Advance wakanipeleka PCM nikaona shule si ndio hii michezo ikaongezeka bana, kuja kushtuka nipo form six tunajiandaa na Mock ndo pressure ikaanza nikiwaza kudifferentiate constant. Nikakomaa dakika za mwisho nikaambulia D ya Pure Math na overall nikalamba Div II 12.

Chuo nilienda zangu Biashara na hadi leo sijajutia maamuzi japo application ya namba naitumia sana na inanibeba. Ila kwenye post graduate ya Actuarial pure ilinisaidia sana pia.
Hiyo post graduate ya Actuarial uliisomea chuo gani mkuu?
 
Japokuwa siyo lazima mtu kujua hesabu, ila huwa napata ukakasi kuona mtoto wa kiume analalama juu ya hesabu ya aina yoyote, bila kujali ni basic, additional au Advanced.

Tukirudi katika mada ni kuwa mimi shule niliyo soma haikuwa na somo hilo, ila nilisoma "Additional Mathematics" kitaa sababu nilikuwa naipenda sana Hesabu.
 
Tcha aliyekuwa akifundisha hakuwa mkali sana na ushawishi,, ivo nikabaki na Basic Math,,

Ndo somo ambalo hata unistukize nlikuwa nalifumua,

Nlikuwa napenda kuanzia kule kwenye marks 40% [emoji23]
 
Japokuwa siyo lazima mtu kujua hesabu, ila huwa napata ukakasi kuona mtoto wa kiume analalama juu ya hesabu ya aina yoyote, bila kujali ni basic, additional au Advanced.

Tukirudi katika mada ni kuwa mimi shule niliyo soma haikuwa na somo hilo, ila nilisoma "Additional Mathematics" kitaa sababu nilikuwa naipenda sana Hesabu.
Sikushangai maana hujawahi kukutana na mtihani wa hili somo.
Wewe unasema kuisomea kitaa wakati watu tumeisoma darasani na tuliifurahia.
Hata na sisi tusingekutana na mtihani basi necta wote tungelifanya.
 
Mitihani yake nimefanya sana na A'level nikasoma Advanced Mathematics na hakuna ugumu wowote katika hesabu kwa ujumla.

Mie sikuwahi soma kabisa Addition, ila waliosoma hiyo addition nilikuwa nawakalisha sana kwenye number elimu za juu.. ingawa sikuwahi kuipenda hesabu kama hesabu.. somo langu pendwa kabisa ilikuwa ni physics na hata sasa hivi naipenda zaidi physics na nilikuwa nainyoosha alie kuwa ananifatia kwa physics na Shadeeya peke ake 😀😀😀😀
 
Hahahaa!! Tunakoelekea utaniumbua rafiki. 😂😂😂

Rafiki we ndio ulikuwa mbaya nazo unakumbuka vile ulikuwa unapata sana tabu kunifundisha na kichwa changu kigumu namna hii. 😉
😀😀😀😀😀..
 
Mitihani yake nimefanya sana na A'level nikasoma Advanced Mathematics na hakuna ugumu wowote katika hesabu kwa ujumla.
Mimi sijawahi kukosa A ya hesabu mtihani wa mwisho.Kuanzia primary,O'level hadi A'level.
Mimi nakuambia kitu nilichokutana nacho wewe unakisia tu!
Halafu maisha ya O'level na A'level kamwe hayawezi fanana.Mimi kuna mtu nimetoka naye shule moja O'level na hiyo addit aliifanya vizuri sana na mtihani wa ACSEE alikosa A mimi nikaipata.
 
Back
Top Bottom