Kuna Wenzangu waliokimbia Additional Mathematics kama mimi?

Naam, Mimi nilisoma hili somo tena kwa ushauri wa rafiki yangu pale Azania,issue ikaja mwalimu wa somo hamna pale Azania ila kwa vile tulitaka sifa basi tukasaini,
Mwl wa Tuition jamaa anaitwa Log man pale mchikichini daah nilipambana nikaenda Jitegemee kulikua na dada nae anasoma hilo somo so alinipigia mapindi, mwisho wa siku Basic Mathematics nilipata A na Additional Mathematics C,
 
Kweli,km mimi chemistry ilinitoa nock out,ila language nilikuwa vizuri,yote maisha huku uraiani tunakutana wote na maisha yanasonga
Mambo ya shule ndio ivyo hakuna mtabe wa kila kitu.. tuna connect connect mwisho wa siku tunatoka mzee
 
Naam, Mimi nilisoma hili somo tena kwa ushauri wa rafiki yangu pale Azania,issue ikaja mwalimu wa somo hamna pale Azania ila kwa vile tulitaka sifa basi tukasaini,
Mwl wa Tuition jamaa anaitwa Log man pale mchikichini daah nilipambana nikaenda Jitegemee kulikua na dada nae anasoma hilo somo so alinipigia mapindi, mwisho wa siku Basic Mathematics nilipata A na Additional Mathematics C,
Ulikuwa vizuri mzee baba.. A ya mahesabu
 
Naam, Mimi nilisoma hili somo tena kwa ushauri wa rafiki yangu pale Azania,issue ikaja mwalimu wa somo hamna pale Azania ila kwa vile tulitaka sifa basi tukasaini,
Mwl wa Tuition jamaa anaitwa Log man pale mchikichini daah nilipambana nikaenda Jitegemee kulikua na dada nae anasoma hilo somo so alinipigia mapindi, mwisho wa siku Basic Mathematics nilipata A na Additional Mathematics C,
Safi sana.
 
Hahaha ilikuwaje?

Mimi hili jina sijui hata maana yake limekuwa na historia tamu kwenye maisha niliyopitia
Lilikuwa la mshkaji wangu
Kuna kijiji kimoja huko mufindi kilikuwa na gari moja tuu, ( bus) na kwenda mjini ilikuwa lazima uwahi mapema sana around saa kumi ili uliwahi,msangarufu
 
Mwaka 1996 tuliletewa mtihani wa kuhitimu kidato cha nne ambao karibu section A yote ilikuwa na maswali ya additional mathematics wakati sisi hatukuwahi kufundishwa additional math. mbona tulijuta hadi mwalimu mwenyewe aliinua mikono. Wengine tulikuja kuponea kwenye section B ndo tukaambilia C wakati katika hali ya kawaida tungepandisha mabanda. Adavance nilienda PCB na sikujutia uamuzi huo kwa sababu hakuna kitu kilichonizingua kama kukaa hapo siku nzima na ku-solve mahesabu.
 
Daa heko mkuu yaani huo mwaka ndio wengine tunazaliwa . Additional mathematics sio rahisi mtu wa basic math kutoboa maana ina chembechembe ya advanced math maana kuna hadi topic za integration, differentiation, na logic
 
Sema ni BAM iliyo na chembe chembe za pure.
Ni A'level tupu.
 
Habarini WaTz wenzangu na poleni sana kwa hili pigo tulilopata karibuni.Tuendelee kumuombea mzee wetu apumzike kwa amani. Na wale wa tarehe 27 tuwaombee wakamilishe furaha yao bila kutokea kwa vurugu yoyote..

Kuna hili somo linafundishwa O'level kwa baadhi ya shule.Linaitwa Additional Mathematics. Ni tofauti na ile Basics ya kawaida.Basi mimi nikachaguliwa kwenda shule fulani hivi inafundisha hilo somo.Nikaenda!

Kufika shule sasa form one hiyo kila mtu anamuonyesha mwenzie yeye ni mwamba hasa upande wa hesabu.Kuna jamaa nakumbuka alikuja na maswali magumu sana ya la saba.Yalikuwa yale ya maduara halafu ndani ya duara kuna duara tena.Halafu ndani kabisa kuna eneo limetiwa kivuli kisha swali ni kutafuta eneo lisilo na kivuli.Kiufupi yalikuwa magumu sana! Sasa mdau akawa anatupa hayo maswali tunakosa anatuelekeza.Ikawa mwalimu asipoingia jamaa anaenda ubaoni anatuamrisha 'fanyeni swali hili'.Na watu tulivyokuwa tunapenda maswali na tupo na hamu ya mitihani basi tunafanya.Wanaopata wanapongezwa na kunadiwa ni vipanga wa darasa.Tunaokosa sasa tunaambiwa ni wazembe hatusomi tumekuja shule kukua n.k.Tukakubali lawama.

Sasa mdau wetu sifa zake zikasambaa.Wakubwa wakaanza kumuuliza dogo unajua maths? Anajibu ndio lete swali.Wakamwambia tulia utafika form 3.Akauliza kuna nini form 3? Akajibiwa 'Additional Mathematics'.Akasema Maths haijawahi msumbua hata kidogo.Kaja darasani kutupa hamasa kuwa kuna somo jipya form tatu la vipanga wa Maths.Akatushawishi tulichukue ili akatukimbize huko.Tukakubali.Tukafika Form Three.

Utaratibu uliokuwepo ni kuwa wanafunzi 40 waliofanya vizuri mtihani wa kidato cha pili ndo wanaruhusiwa kusoma hilo somo.Japo kama upo kwenye hao top 40 ni hiari yako kulisoma au kuliacha.Jamaa nakumbuka hakuwa miongoni mwa hao top 40.Alilia sana yaani.Kaenda kwa mtaaluma kamlilia wampange kagomewa.Ila baadaye mwalimu wa somo kaitwa na uzuri alikuwa anaona juhudi zake hivyo akamruhusu.Uzuri kuna mtu miongoni mwetu hakutaka kusoma hili somo kwa hiyo wakabadilishana jamaa akaingia kundini.
Mtihani ukaja.

Hili somo ni kawaida wa kwanza kupata 98 na wa mwisho kupata single digit ni kawaida sana.Maana mwanzo mnaanza wote 40 ila wanaofanya necta ya form four hawazidi 18.Tukafanya mtihani matokeo yakaja.Mimi nikapata 55.Halafu nikasikia alikuwa anaongeza maksi kumi maana wengine walifeli sana na hakutaka kutukatisha tamaa.Kweli nikahesabu nikakuta nimeongezewa kumi.Nikajiuliza ndo paper ya kwanza tu hii! Ila nikasema wacha nikomae.Na uzuri mwalimu alikuwa na mtindo wa kurudia rudia maswali nikasema sio mbaya.Jamaa yule akapata 70.

Mtihani wa terminal ambao ndo mwamuzi wa alama utakazopata nikakomaa usiku kucha na hilo somo.Uzuri walipendelea kuliweka peke yake siku nzima.So sikuwa na kingine cha kusoma tofauti na hilo.Soma sana pitia mitihani nikalala saa saba.Nilichelewa kujiandaa nikajikuta nachelewa chumba cha mtihani. Nilivyoingia nikakuta wenzangu washaanza na msimamizi hayupo japo siti yangu ilikuwa na karatasi tayari.Nilichofanya nikajongea taratibu kwenye siti yangu nikayacheki maswali huku nimesimama.Kwa haraka haraka sikuona swali nililoweza kulifanya.Kufunua nyuma swali la mwisho nikakuta lile la seti tatu nalo nilifahamu baadhi ya vipengele nisingepata lote.Cha kufanya nikarudisha kalamu yangu mfukoni nikatoka nje.

Nikasikia wadau wanacheka sikujali.Nikamfuata mwalimu wa somo nikamwambia ticha mimi naumwa hivyo sitafanya pepa.Akakataa kunisikiliza maana aliniona nacheza boli jana yake. Nikamwambia nimeamka asubuhi najisikia vibaya nimeharisha sana na kichwa kinauma.Akasema mimi mjanja ananijua yaweza kuwa nimeingia chumba cha mtihani nikakuta mambo mazito nikatoroka.Akasema twende room la pepa.Tukaingia akakuta mapepa yaliyowekwa kwenye siti yangu yapo vilevile. Akauliza huyu vipi hajaingia humu?

Wadau wakasema hajaingia.Kauliza msimamizi akajibu hajaniona mtu kama mimi.Nikapona tukatoka.Sema nikamwambia afanye kama sijawahi kugusa pepa la 'aditi' maana asingefanya hivyo angegawa ile maksi yangu ya awali kwa nusu na hasara ingekuwa kubwa zaidi.Maana walichofanya ni kuchua alama za nusu muhula wanajumlisha na za mtihani wa muhula kisha wanagawa kwa mbili.Sasa mimi mid term nina 55 ila terminal sikufanya hivyo 0. Hapo napata 27.5(F).Ticha akasema kunijumlishia ama kutokunijumlishia ni juu yake hivyo nisimpangie.

Matokeo yakaja nyumbani Mzee anang'aka napataje F ya hesabu.Kuyacheki nakuta alinijumlishia bhana.Nikamwambia Baba sio hesabu hiyo.Akasema namdharau hajui maana ya Mathematics.Nikakubali lawama hiyo siku.Japo Basic Mathematics nina B ila Additional Mathematics nina F.Yakapita nikarudi shule.

Wakaanza kutugawia mapepa tuliyofanya kabla hatujafunga.Yule ticha akaanza kugawa mapepa yake.Akaanzia wa kwanza kuja wa mwisho halafu kazipangilia.Wa kwanza 98%! Watu wanasoma bhana! Kaendela hivyohivyo kuita karatasi.Tukaona yule jamaa yetu hatajwi,tukaanza kushangaa.Kumbe mdau kavuta mikia ya wenzie.Alipata 19%.Tukazuia vicheko tukasubiri ticha amalize 'correction' hadi alipotoka.Naye jamaa akanyanyua mikono hiyohiyo siku.

Tulianza 40 kwa mbwembwe na mizuka ya ajabu ila waliofanya CSEE ni 18 tu.Tena ni wale wapole tu ila sisi waongeaji wote nje.

Hili somo ni gumu japo linasaidia sana A'level.
Nimemaliza shule sec 1991 ( wengi wenu humu mlokua viunoni nikiangali cheti changu cha o level Nina F ya addition nakuficha binti yangu asikione naumia aisee
 
Nilitamani sana kufanya hilo somo O’ level. Sikupata nafasi hiyo tu.
 
Back
Top Bottom