Kuna wengine kwenye picha hii bado wanataka tuwape uongozi!

Kuna wengine kwenye picha hii bado wanataka tuwape uongozi!

Wanasiasa hasa wa Afrika ni moja ya watu ambao hawana aibu za kisiasa. Tatizo kuu la kukosa aibu ni kwa sababu wanazifanya siasa kama sehemu ya ajira na kujiaminisha kama ni kipaji.

Walioweka dhana ya ukomo wa madaraka ya wanasiasa hawakuwa wajinga kwa sababu walijua athari za kuwepo wa wanasiasa wanaodhani siasa ni ajira na kipaji.

Fikiria mtu ambaye amezaliwa na kukuta Mwl, Nyerere ametangulia mbele ya haki kwa sasa ana miaka 20. Mtanzania huyu kwa Katiba yetu anatatakiwa kuwa mwakilishi wa wananchi lakini anakosa nafasi kwa sababu ya ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa wanaodhani siasa ni ajira na kipaji.

Nakumbuka Mwanzilishi wa Tuzo ya Utawala Bora Afrika, Mo Ibrahim aliwahi kuligusia suala hili aliposema, Bara la Afrika ni changa ambalo lina vijana wengi wenye umri wa miaka 20 lakini viongozi wake wengi ni wazeee sio wa miaka pekee bali hata kifikra.

Ukiangalia takwimu za Sensa ya Mwaka 2012 utagundua kuwa Watanzania wenye umri wa miaka 0-20 ni asilimia 54.2, wakati wenye umri wa miaka 20-40 ni asilimia 28.5. Hii ina maana kuwa Watanzania wenye umri wa miaka 0-40 ni asilimia 82.5.

Leo unakuta mtu aliyewahi kuwa Mbunge au kwenye Balaza la Mawaziri wa serikali ya Rais Nyerere bado anataka tuendelee kumpa uongozi wa kisiasa! Hivi sisi ni wajinga au wapumbavu?

Kinachoshangaza zaidi unakuta kijana wa umri wa miaka 20 anapanga foleni kumpa kura mtu aliyewahi kufanya kazi ya kisiasa kwenye serikali za wakati wa Rais Nyerere!

Jaribu kufikiria ni wananchi wangapi wenye umri wa miaka 40 kushuka chini ambao wako kwenye uongozi wa kisiasa nchini?

Bila kuiondoa dhana ya ‘’genontocracy’’ tutaendelea kukumbatia wanasiasa wanaodhani siasa ni ajira na kipaji ambao hata fikra zimezeeka!

img-20190115-wa0195-jpeg.995447
Kawawa na pierre liquid ni mapacha?
 
Mkuu;
Zionyeshe hizo chuki zake!
Mimi nadhani amejenga hoja kulingana na mtazamo wake lakini kikubwa zaidi aliwataja wote wamekuwa kwenye uongozi wa kisiasa za kuchaguliwa katika cheo kimoja kwa miaka zaidi ya 15
Wa upande mmoja awataje hadi kwa majina alafu wa upande wa pili unajificha kwenye chama kizima mfano magufuli na mbowe ni nani mkongwe kwenye siasa
 
Tatizo linaanzia kwenye vyama vijana wakijitokeza kugombea wanakatwa mapema.maana huko kwenye vyama ndio kuna zile kamati na wameajazana wao.
Halafu na bado kama ulivyosema vijana hao hao wanapanga foleni kulichagua lizee.
Tatizo kuu ni vijana kutojua umuhimu wao!
 
Hao vijana kutoka miaka 20 hadi 40 hawana nia madhubuti na siasa. Wachache sana, kukuta kijana chini ya miaka 40 anayo interest na siasa ni shughuli
Ninakubaliana na maoni yako.

Kinachotakiwa ni kubadilisha mentality.

Vijana wengi nadhani bado wanadhani uongozi wa kisiasa niwa wazee pekee!
 
Angalia Mtu Kama Sumaye Bado Linataka Vyeo Tena Vya Upinzani Duh Vijana Watafanya Kaz Gan?
In fact ,hadhi na heshima ya Sumaye inapanda.
Inaonyesha kuna kitu anakiamini na yupo radhi kupoteza kila kitu, hata maisha kwa kukipigania kitu hicho.
Achukue tu muda ajieleze vizuri, watu watamuelewa sana.

Hii dhana ya umri katika siasa ni gheresha tu isiyo na maana yoyote. Tanzania haina tofauti yoyote na mataifa mengine duniani.
 
Tatizo linaanzia kwenye vyama vijana wakijitokeza kugombea wanakatwa mapema.maana huko kwenye vyama ndio kuna zile kamati na wameajazana wao.
Halafu na bado kama ulivyosema vijana hao hao wanapanga foleni kulichagua lizee.
Basi pendekeza pawepo na vyama vya vijana, wanyukane na vyama vya wazee.
 
Mkuu umesema vyema, kuna wabunge kwa mfano wamejimilikisha majimbo.miaka yote yumo tu...
 
Back
Top Bottom