Kuna wengine kwenye picha hii bado wanataka tuwape uongozi!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,929
2,000
Wanasiasa hasa wa Afrika ni moja ya watu ambao hawana aibu za kisiasa. Tatizo kuu la kukosa aibu ni kwa sababu wanazifanya siasa kama sehemu ya ajira na kujiaminisha kama ni kipaji.

Walioweka dhana ya ukomo wa madaraka ya wanasiasa hawakuwa wajinga kwa sababu walijua athari za kuwepo wa wanasiasa wanaodhani siasa ni ajira na kipaji.

Fikiria mtu ambaye amezaliwa na kukuta Mwl, Nyerere ametangulia mbele ya haki kwa sasa ana miaka 20. Mtanzania huyu kwa Katiba yetu anatatakiwa kuwa mwakilishi wa wananchi lakini anakosa nafasi kwa sababu ya ubinafsi wa baadhi ya wanasiasa wanaodhani siasa ni ajira na kipaji.

Nakumbuka Mwanzilishi wa Tuzo ya Utawala Bora Afrika, Mo Ibrahim aliwahi kuligusia suala hili aliposema, Bara la Afrika ni changa ambalo lina vijana wengi wenye umri wa miaka 20 lakini viongozi wake wengi ni wazeee sio wa miaka pekee bali hata kifikra.

Ukiangalia takwimu za Sensa ya Mwaka 2012 utagundua kuwa Watanzania wenye umri wa miaka 0-20 ni asilimia 54.2, wakati wenye umri wa miaka 20-40 ni asilimia 28.5. Hii ina maana kuwa Watanzania wenye umri wa miaka 0-40 ni asilimia 82.5.

Leo unakuta mtu aliyewahi kuwa Mbunge au kwenye Balaza la Mawaziri wa serikali ya Rais Nyerere bado anataka tuendelee kumpa uongozi wa kisiasa! Hivi sisi ni wajinga au wapumbavu?

Kinachoshangaza zaidi unakuta kijana wa umri wa miaka 20 anapanga foleni kumpa kura mtu aliyewahi kufanya kazi ya kisiasa kwenye serikali za wakati wa Rais Nyerere!

Jaribu kufikiria ni wananchi wangapi wenye umri wa miaka 40 kushuka chini ambao wako kwenye uongozi wa kisiasa nchini?

Bila kuiondoa dhana ya ‘’genontocracy’’ tutaendelea kukumbatia wanasiasa ambalo kifikra wamezeeka lakini wanaodhani siasa ni ajira na kipaji!

img-20190115-wa0195-jpeg.995447
 
technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,909
2,000
Leo Umeongea Jambo La Msingi
Watu Kama Wakina Mbowe, Seif, Lipumba, Mrema,na Wazee Kibao Ndani Ya Ccm Wanatakiwa Kupumzika Vijana Wapo Wengi Sana .

Huwa Nashangaa Sana Kusikia Mfuasi Wa Chadema Anasema Mbowe Yupo Imara ! Uo Uimara Unapimwaje ? Chama Kinasinyaa Kinapoteza Falsafa Watu Eti Yuko Imara!

Lazima Kuwepo Na Utashi Wa Kisiasa Kama Ni Mrithi Intelijensia Ya Chama Ipo Na Wanachama Wanajua Wanamtaka Nani .

Lazima Tukubali Changamoto Mpya Unakuta Jitu Lina Miaka 65 Bado Linajipendekeza Kwa Rais Kupewa Cheo Wakati Yupo Serikalini Zaidi Ya Miaka 40!!

Angalia Mtu Kama Sumaye Bado Linataka Vyeo Tena Vya Upinzani Duh Vijana Watafanya Kaz Gan?
 
Mkuu;
Maoni yako yamenifanya nicheke!

Unakuta vijana wanajipanga kwenda kumpigia kura mbunge ambaye amekuwa bungeni toka awamu ya kwanza!
 
Tajiri mpole

JF-Expert Member
Apr 15, 2018
1,683
2,000
Leo Umeongea Jambo La Msingi
Watu Kama Wakina Mbowe, Seif, Lipumba, Mrema,na Wazee Kibao Ndani Ya Ccm Wanatakiwa Kupumzika Vijana Wapo Wengi Sana .

Uwa Nashangaa Sana Kusikia Mfuasi Wa Chadema Anasema Mbowe Yupo Imara ! Uo Uimara Unapimwaje ? Chama Kinasinyaa Kinapoteza Falsafa Watu Eti Yuko Imara!

Lazima Kuwepo Na Utashi Wa Kisiasa Kama Ni Mrithi Intelijensia Ya Chama Ipo Na Wanachama Wanajua Wanamtaka Nani .

Lazima Tukubali Changamoto Mpya Unakuta Jitu Lina Miaka 65 Bado Linajipendekeza Kwa Rais Kupewa Cheo Wakati Yupo Serikalini Zaidi Ya Miaka 40!!

Angalia Mtu Kama Sumaye Bado Linataka Vyeo Tena Vya Upinzani Duh Vijana Watafanya Kaz Gan?
Sasa Rika LA Mbowe na jiwe si sawa tu...Tena Jiwe mzee,kwanini yeye hujamsema?
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,929
2,000
Hizo chuki binafsi ulizo nazo kwa wapinzani wa kisiasa zinakusaidia nini?
Mkuu;
Zionyeshe hizo chuki zake!

Mimi nadhani amejenga hoja kulingana na mtazamo wake lakini kikubwa zaidi aliwataja wote wamekuwa kwenye uongozi wa kisiasa za kuchaguliwa katika cheo kimoja kwa miaka zaidi ya 15
 
RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
16,782
2,000
Tatizo linaanzia kwenye vyama vijana wakijitokeza kugombea wanakatwa mapema.maana huko kwenye vyama ndio kuna zile kamati na wameajazana wao.
Halafu na bado kama ulivyosema vijana hao hao wanapanga foleni kulichagua lizee.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,929
2,000
Kuna vijana wengi wamepata vyeo lakini mambo yao hata hao waliopo kwenye picha wangekuwa Hai wote wasingewafikia hata kwa asilimia.chache.
Mkuu;
Hao vijana wengi umewapimaje? unadhani wakati wao wa utawala hawakuwepo hao vijana ambao mambo yao hayakuwa mazuri?

Huwezi kuchukua dhana ya ''samaki mmoja akioza wote wameoza'' halafu ukaiweka kwenye uongozi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom