Chrysanthemum
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 1,807
- 6,561
Halafu vyeo na deals nzuri nzuri wanakula wavivu 😃😃 haya maisha bhana yana njia nyingi za kutushangaza !!!
Hivi watumishi wa umma hasa hawa wa kuajiriwa huwa wanaapa viapo kweli? Huwa wanaapa mbele ya nani?Kweli kuna watumishi waliapa kiapo cha haki kabisa
Kweli kabisa mkuu, japokuwa mimi si joseNikisoma shuhuda kama hizi huwa napata amani kidogo, maana kwa kweli nilisha generalise kuwa watu ishi wote wa umma ni mashetani, hasa polisi, mahakama, uhamiaji, na hospitalini , huko kote niliishia kupata si huduma baki adhabu kali iliyosababisha nijute kuzaliwa Tanzania, ila kama bado kuna watu wema hata wachache kama huyo Jose nawa ombea kwa Mungu awape mlima wa baraka, si rahisi kuwa mwema kwenye mfumo uliooza, hata kama mtoa mada ndiye Jose mwenyewe atakuwa anaiishi hadithi yake hii tamu yenye kutupa matumaini sisi tulio wahitaji, Mungu akubariki sana Jose.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Hawa ni kuwabainisha kama hivi ndo dawa yao, tusikae kimyaMi nasema ukweli! Kuna Mama mmoja pale Baraza la Aridhi na Nyumba Tanga anajiita D. W. Mangure ndiyo Mwenyekiti pale, yule Mama ni mlaa rushwa sana,na anapenda kuendesha Magari makubwa Kama Alfadi!! Naomba Takukuru Makao makuu wamchunguze kimya kimya, hasa kwenye hukumu zake anazotoa, huwa anawa fever sana wenye pesa bila hata ya aibu! Yaani hukumu zake zinatofautiana hadi na maoni ya Wazee wa Baraza lake!!
Aisee mungu amsaidie yule brohDaah mwambie awe makini maana kizuri hakidumu
Kweli aisee. Hata mimi nilikutana na Mwl kwenye shule moja ya sekondari kule Kigoma aisee alikuwa Second Master jamaa anapiga kazi hadi nilimkubali. Alinipa moyo sana. Na ilikuwa Raha sana kufanya kazi na yule mtu. Nilishamsahau jina maana ni kitambo sana.Habari wakuu,
Kweli nimeamiani kwenye kundi la kenge huwezi kosa na mamba. Na pia samaki mmoja akioza si kwamba wote wataoza.
Nimeongea hayo kwa kujithibitishia kwa kuona baadhi ya watumishi wa umma wanafanya kazi zao kwa umakini na kwa weledi mkubwa sana. Kweli kuna watumishi waliapa kiapo cha haki kabisa.
Nilienda almost mara tatu pale branch ya RITA manispaa karibu na uwanja wa TAIFA , nikakutana na mwamba mmoja anaitwa Jose, huyu mwamba anapiga kazi kisawa sawa yaani, yaani yuko tayari hata asile mlo wowote ule ila ahakikishe wateja wake wote wamepata huduma.
Mwamba mcheshi na akiwa kazini anapiga kazi like hakuna kesho. Jamaa hana dharau na sio mtu wa kufokea wateja kama wafanyavyo baadhi ya watumishi. Pia mwamba ana nidhamu na ni mtu makini sana.
Kuna siku jamaa alizidisha muda wake wa kazi kutoka saa 6 mpaka 12 jioni, kwa kuhudumia wateja. Huyu mwamba aliniaminisha kuwa si watumishi wote ni wahuni. Bali kuna wapiga kazi kweli kweli.
Hongera sana mwamba kama umesoma uzi huu basi big up man, soon utatoka sehemu moja na kwenda nyingine kaka
Wakati wewe uko mwaminifu ktk kazi wengine wako bize na connection na mafisadi tu. Na hapo ndio unaonekana mkorofi 😅😅Cha ajabu katika utumishi wa umma ukiwa mchapakazi unaonekana ni tatizo.....Tuna safari ndefu sana.
Bora tuwe tunawachana hivyo hivyo maana Takukuru haina kaziMi nasema ukweli! Kuna Mama mmoja pale Baraza la Aridhi na Nyumba Tanga anajiita D. W. Mangure ndiyo Mwenyekiti pale, yule Mama ni mlaa rushwa sana,na anapenda kuendesha Magari makubwa Kama Alfadi!! Naomba Takukuru Makao makuu wamchunguze kimya kimya, hasa kwenye hukumu zake anazotoa, huwa anawa fever sana wenye pesa bila hata ya aibu! Yaani hukumu zake zinatofautiana hadi na maoni ya Wazee wa Baraza lake!!
Inashusha sana morali ya kazi, 2021 ilikua ndio mwisho wangu kufanya kazi kama punda....haitakaa ijirudie labda kazi zangu binafsi ila sio za umma, nilijifunza mengi sana ukifanya kazi kwa kujitoa unakua ni tatizo.Wakati wewe uko mwaminifu ktk kazi wengine wako bize na connection na mafisadi tu. Na hapo ndio unaonekana mkorofi 😅😅
Ndiyo unless uwe mtu wao( satan company)Inashusha sana morali ya kazi, 2021 ilikua ndio mwisho wangu kufanya kazi kama punda....haitakaa ijirudie labda kazi zangu binafsi ila sio za umma, nilijifunza mengi sana ukifanya kazi kwa kujitoa unakua ni tatizo.
Kuna umuhimu mkubwa sana wa Mama kua mkali kwa Watoto wake ambao ndiyo Watumishi wa Umma, Mtoto ukimdekeza sana anaharibikiwa, Mama ajaribu kua mkali kidogo Kama alivyokua Marehemu Baba!!Kichefuchefu kipo Manispaa ya Kinondoni aisee, unaenda unahitaji kushughulikiwa jambo lako kupata jibu mtu hadi amalizie kutuma emoj kwanza...![]()
Mtaje kwa majina Mkuu.Kuna dada mmoja wilaya flani mkoa wa Pwani asee dada anapiga kazi sana Mungu ambariki sana.
Unamjua jose mwenyewe pale RITASema Jose unatafuta cheo sana, unahisi Alex akiona hii post ndio atakupandisha? Pale pamekaa kikabila mchizi wangu, we komaa na mishe zingine ila usitarajie kutoka kupitia hiyo kazi