Kuna watu waliowahi kukataa uteuzi wa Rais?

Haijawahi kutokea ndo mana hata JAMES MBATIA pamoja na kumpinga sana kikwete lakini alikubali uteuzi wake
 
Mbona hao ni wengi hasa kwa nafasi ya ukuu Wa wilaya na mkoa na vyeo vingine visivohitaji utaalam
 
Marehemu Jaji Mkude alikataa uteuzi wa kuwa Jaji wa mahakama kuu zaidi ya mara mbili, na sababu kuu ilikuwa afya ya wazazi wake ilihitaji uangalizi wake wa karibu sana, asingeweza kutimiza majukumu makubwa ya nafasi ya ujaji katika hali ile.
Ahsante Sana Mkuu! Ilikuwa kwa kipindi cha Rais yupi Mkuu?
 
Siyo lazima lakini busara na utaratibu inamtaka mwenye appointing authority kaniuliza kwanza anayetala Kim appoint ili asije kumdhalilisha
 
Mbatia pamoja a kuiponda serikali ya ccm chini ya jk, alikubali kuwa mbunge wa viti maalumu. Usicheze na nafasi za kiteuliwa 1/100 ndio wanakataa.
 
Mzee wa 'wapigwe tu' Aliukataa uwaziri mkuu alipoteuliwa kwa mara ya pili. Maana aliona 'Dege John' kamdharilisha kwa kumpiga chini kimya kimya bila ya kumuambia akataka kumuweka Mkulo nadhani. Wazee wa Chama na nchi wakaingilia na kumpiga stop 'Dege John', kazi ikawa kumshawishi Mzee wa 'wapigwe tu' kukubali tena ule uteuzi, jamaa aligoma kabisa kabla ya Lodi Lofa kutuma amri kupitia yule mzee aliyehudumu kwenye serikali zote kasoro ya awamu ya tano.
Si mnajua tena kuwa Lodilofa yeye hayo mambo ya kuwa Romantic hanaga muda nayo, yeye ni amri tu, sema uzuri wake yupo very reasonable.
 
Henry Mapolu alikataa kuwa DC enzi za Mwinyi au Nyerere,Mapolu alikuwa mhadhiri UD baadaye akawa mwanaharakati .
Kuna mtu pia aliwahi kukataa U RC enzi za JK,JK mwenyewe alisema ila hakumtaja jina.
Kuna mwanamama (jina nimelisahau) pia alikataa nafasi ya u DC enzi za Mkapa,alimwambia mkapa alipokuwa anafanya kazi kuna mradi anausimamia na ulikuwa unakaribia kuisha kwahiyo ni bora aumalizie Mkapa alimuelewa akateua mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom