Kuna watu tuliumbwa kupishana na gari la mapenzi

Naandika kwa uchungu sana. Huwa nikipenda mwanaume mmoja nampenda huyo huyo na siwez kumcheat labda anizingue. Mwanaume ambae nilijua tutamaliza wote maisha yaliyobaki hapa duniani ameniumiza sana. Ningekua labda mbaya nisingeumia sana. Ila hata bwana angu huwa ananiambia haamini mimi kumpenda yeye. B umeamua kuniumiza moyo wangu kwa mara nyingine. Nakuombea mabaya na huyo mwanamke ulie nae. Na namuomba Mungu anisikie kilio changu.
Niamini Mimi nisemaye
Karibu kwangu hutojuta kupenda
 
Pole shoga angu...kosa kubwa ulilofanya ni kumuonesha huyo mwanaume kuwa unampenda sana! Bonge moja la mistake...na usipojirekebisha itakucost...

Mi nimejifunza asee ukinipenda nami ndo ntakupenda, once nitakapohisi janja janja Usain Bolt anasubiri ...hakuna kutesana hapa!
Ikitokea Jamie nakupenda sana but sitaki kukionesha kuwa nakupenda sana? Kwa kuogopa kuumizwa?
Basi siku hizi mapenzi so mapenzi tena
 
Pole kwa hayo mamito

Jitahidi kumsahau na hakikisha penzi lako humuachi nalo yeye baki na penzi lako jipe muda na ukimpata mtu jitoe kwa dhati na wala usiape kutopenda tena, kupenda kuna raha yake

Kingine cha mwisho punguza minato uzuri na mvuto wako sio kigezo cha kutosalitiwa jishushe kwa umpendae wanawake wazuri wamejaa kila kona lkn jiulize kwa nini wengi wao wameishia kujiuza

Nina mashangazi zangu ni wazuri kuanzia juu mpk chini wana maumbo masogange cha mtoto lkn wapo tu wanaranda kitaaa haya mambo ya kujiona uzuri yanatucost sana ndo utashangaa unaachwa na hayo yote yako anafatwa mwanamke wa kawaida asie na mvuto na bwana akatulia kwake
 
Kosa kubwa tunalolifanya sisi wanadamu n kuhisi labda ukimfanyia mtu wema sana ..na ww atakufanyia hvyo hvyo ... .na ndo maana ikiwa kinyume na matarajio huwa tunaumia ..hvyo hvyo kwenye mapenz we don't need to expect to much from our partners
Ukiyafanya haya maisha mbona mepesi???
 
mwenza tutake radhi bwana kwa hiyo wabaya hatuna haki ya kuumia au halali yetu kuumizwa? Mungu anakuzoom
 
Pole sana. Hata mabinti nao hawaamini vile vile kuwa kuna wanaume tuliojituliza na tukipenda hatutamani kwingine. Sitaki kuamini kuwa duniani hakuna hata mtakatifu mmoja sawa.
 
Mzigua,mimi sina maneno saaana,njoo kwangu tuyajenge,nakuhakikishia hutojuta,
nasubiri pm yako tu,
 
Back
Top Bottom