Kuna wanawake wana moyo wa kuvumilia...

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
9,016
16,150
Siku zote najinasibu ni mtu wa gambe, yes napiga tungi kwelikweli na hapa napost hii. Nimerudi nimemkuta mke wangu Muanglican anasali rosali. Nimefunguliwa na Dada Wa kazi, kanipakulia mke yupo tu chumbani.

Naingia chumbani ananiambia “NAJUA UNA MTOTO NJE YA NDOA YETU, TUMEKAAA MIAKA MINNE HATUJAPATA MTOTO. Nimekusamehe” Nilikuwa namkuta hivyo tu kumbe ana maombi yake. Leo kaniletea vipimo ana mimba na anamjua mtoto wangu wa nje na ameongea na yule mama akijifanya dada yangu na kamkatia bima kupitia mshahara wake

Ananipendaje Huyu. Yote haya ananiambia usiku huuu nimerudi mtingo “Usipolewa Mme wangu ni mstaarabu Sana ila Ukilewa tu hauchagui. Nimekukuta na watoto wawili (niliwapata ujanani) umeniongezea mwingine. Simwambii mama nitamlea mama Wangu”

Wa nje ndio mdogo, ndio amezaliwa na yeye ndio mjamzito.

Yaani pombe imekata paaaaaa.
 
Nikuhongereshe kamanda. Umepata mke mwema sana. Ingekuwa hawa ninaowafahamu, saa hii mtaa mzima ungekuwa umejaa hapo nyumbani kwako. Mpende sana huyo mke aisee na jitahidi sana uache michepuko sasa. Umepewa nafasi nyingine. Rudi kwa Mungu sasa ili ndoa yako iendelee kubarikiwa
 
Kuna wanawake Mungu awabariki sana, ni nadra kwa miaka ya sasa kupata mwanamke kama huyo wapo watakaomshangaa anangoja nini lakini ni upendo tu. Upendo una kila kitu ndani yake, mwanamke wako anajua kukusitiri na kukuvumilia sana hapendi mpasuko katika familia cha muhimu fanya ubadilike mkuu.
 
Kua karibu na mkeo duuh tunakwama wapi huo mda wa gambe kunywa ukiwa nae home
 
Kwa sisi sisi wanawake Hawa Hawa Tena wakibongo?

🤣🤣🤣🤣🤣.

Time will tell.
 
Hapa ingelikuwa mwanamke kapata mimba nje ungesikia mke wangu malay....a namrudisha kwao. Lakini chalii kaleta mtoto nje ya ndoa anasema mke mwema, nasubiri mrejesho wa hio mimba ya wife nae.🤣🤣


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
Nna uhakika ni wangu ..maana tumeenda Pamoja vipimo vyote... Na tukapewa tarehe ... Uzuri zaidi zile siku7 -
zote tumezimalizia msibani ... Kwa kuwa mimi ndio nimejenga pale ukoooni ... Alikkuwa analala chumbani .. Akiwa Wa kike Ntamuita Nyakiro akiwa Wa kiume ntamuiita Nyakiroto ..
 
Back
Top Bottom