Kuna Wakuu wa Mikoa na kuna Amos Makalla. Rais Samia anapaswa kujiuliza mambo mengi

Kusifiwa kwa Rais kuliasisiwa awamu ilopita na tukajua itakuwa nayo imezikwa rasmi kama jamaa kumbe bado inaendelea kufanyika bila kukemewa.

Haifai kiukweli.

Na inchangiwa na mapungufu ya kikatiba ya Viongozi wengi kupatikana Kwa kuteuliwa na mtu mmoja tu.

Kwa hiyo inachukuliwa kama vile ni hisani ya yule mtu alowateua.

Wengine hawajui kuwajibika vyema ktk kutumikia watanzania badala yake wanaficha udhaifu wao Kwa kujikita kwenye kumpamba na kumsifia alowateua kwa hisani.
 
Hivi nyie mnajua utamu wa Msosi?

Makala alikua huko mvomero akapewaU RC kwanini asisifu.
 
Hii habari imenichekesha sana maana kimsingi jana nimeota niko na mama Samia somewhere tumeenda kwa ziara ya kimya kimya on a private car nakumbuka ilikuwa subaru nikiwa na mdogo wangu flani.

Maza alikuwa ni mkaksi kichizi sema tuliishi nae kibingwa. Tulifika lile eneo la ofisi tukaingia ndani akawa anawahoji watumishi flani boss wao alikuwa hayupo akapigiwa simu akawa hajapokea maza akamaindi kinoma.

Kupiga tena ndio akapokea akaahidi anakuja haraka. Baada ya muda tumetoka tupo ndani ya gari maza alikuwa amekaa siti ya dereva mwenyewe akawa anapiga nyimbo zake za ajabu ajabu akaniomba nimuwekee nyimbo mpya tukirudi mjini.

Sasa ile namuuliza master plan ya pale tunafanyaje maana tushakaa sana parking jamaa haji vipi ataendesha tena mda wa kurudi home. Maza kamaindi kaanza rudisha gari kwa reverse kwa speed kubwa kuashiria kakasirika na lile swali 😂😂😂 ikabidi nimtulize nikampokea uskani.

Nikamrudisha tena pale nikawashusha na mdogo wangu nikawaacha mie nikaendelea na harakati zangu.
Umeamkaje ndugu dereva,au ndoto inaendelea 😂
 
RC wa Dar na Dodoma naona ni miongoni mwa maRCs wanaofanya kazi vizuri na kwa akili .

Hapo kwenye kusifu na kuabudu ndipo wanapaswa kujirekebisha kwa kuacha kufanya hivyo!

Badala yake wajikite kwenye kutumikia watanzania kwa tija kubwa endelevu na kuondoa kero ikiwemo migogoro ya ardhi Kwa wakati hasa Mkuu wa mkoa wa DSM.

Shughulikia kutatua migogoro ya ardhi eneo la Mbopo in particular kwenye Kata ya Manwepande.

Ondoeni wale wahuni mnapata kigugumizi gani?

Juzi kaenda DC Gondwe Kawapa siku 7 waondoke.

Je mmejipangeje iwapo baada ya siku 7 watakuwa hawajaondoka?

Ifike mahali hili swala litatuliwe na kuisha ibaki historia.

AIONE na kuisoma :

1. RC Dar

2. DC Kinondoni

3. Wahusika wengine
 
Amos Makalla kwa muda mrefu amekua amitumia nguvu na sifa kwa raisi na pengine hata Raisi mwenyewe hafurahishwi na hilo Ila tu hawezi kusema. Ili Raisi afanye vizuri zaidi anapaswa kuelezwa zaidi changamoto kuliko sifa.
kama ulikua hujui ni kwamba makala na kangi ni mama mmoja baba tofauti.

Nawasilisha.
 
Hivi kuna kusifiwa zaidi ya kuambiwa Mheshimiwa mungu? Hivi kuna kusifiwa zaidi ya kuambiwa "kwamba kwa mambo uliyofanya inatakiwa Mungu akushukuru"..na anayeambiwa hivyo anachekelea....acha bwana wewe mwendazake alikuwa anapenda sana kusifiwa.
Huu ulikuwa ugonjwa wa awamu ya mapambio,na bado ugonjwa huu hauja toweka,zipo dalili za kuibuka Kwa Kasi mpya.
 
Raisi anapoteua wasaidizi, hateui wawe kazi yao kumsifia na kumpamba kupitiliza. Bali huwateua kwa lengo la kumsaidia kazi na kuleta maendeleo.

Amos Makalla kwa muda mrefu amekua amitumia nguvu na sifa kwa raisi na pengine hata Raisi mwenyewe hafurahishwi na hilo Ila tu hawezi kusema. Ili Raisi afanye vizuri zaidi anapaswa kuelezwa zaidi changamoto kuliko sifa.

Speech ya leo huenda ikamuacha na maswali pia raisi, maana mkuu wa mkoa amesifia hadi akakosa maneno akaanza kucheka/kutabasamu.

Ukiachana na hayo Amos Makalla amesema majina ya miradi iliyobakia ipewe jina la Samia. Si Jambo baya ila kuenzi kazi nzuri ya raisi Wala sio kuipa miradi majina yake bali kumsaidia kulinda miradi hiyo iwe endelevu.

Mkapa alijenga miradi mingi kwa miaka 10, Ila aliishia kuwekwa jina lake kwenye miradi miwili: Daraja la rufiji na uwanja wa Taifa.

Kikwete alijenga miradi mingi kwa miaka 10, Ila naye majina yapo Daraja la malagarasi na taasisi ya moyo.

Magufuli alijenga miradi mingi kwa miaka 5, Ila majina yake yapo Daraja la kigongo na Standa ya mabasi mbezi.

Hii tafsiri yake raisi kufanya vizuri sio kuipa miradi majina yake. Kwa maana ingekua hivyo nchi nzima ingejaa majina ya mkapa, kikwete na Magufuli.

Leo mkuu wa mkoa anataka SGR na flyover ipewe jina la Samia.

Wasaidizi wa raisi, msaidieni raisi kulinda miradi na kuifanya kuwa endelevu. Hiyo ndio njia pekee ya kumshukuru kwa alichofanya na sio kuipa majina.
mapokeo ya kusifiwa hutegemea akili, busara na hekima za msifiwa kama hakatazi hilo, na kama hana sifa au umaarufu na uwezo binafsi au ushswishi wa watu, kisiasa, kiushindani, au Kama mtaji kwa utamaduni wao kiutendaji na utopolo wa kisiasa tarajia hilo.

Makala ni Mwanaume masalia usihangaike nae ana nena injili ya masalia waliookotwa jalalani kabla hawajaoza.
 
Huu ulikuwa ugonjwa wa awamu ya mapambio,na bado ugonjwa huu hauja toweka,zipo dalili za kuibuka Kwa Kasi mpya.
Kusifiwa kulianza enzi za Kikwete na wanamtandao wake, alisifiwa sana tena kiutopolo topolo tu, ila awamu yake siasa huru ilikuwepo sana tu,

Magufuli akaiga kusifiwa kipumbavu zaidi na kujitukuza huku akijenga kisiwa huu upumbavu ulifedhehesha sana awamu ya Magufuli.
 
Halafu kosa ni pale utakapowambia ukweli wanatukana kuliko mpiga debe wa stendi.
Hahahaha.. wengi wao matusi, majungu na fitna ndio ajira yao. Yani wanalipwa kulingana na aina ya tusi, fitna au majungu utakayoandika hapa JF. Hata mleta uzi huu tayari ana uhakika wa kulipwa kwa sababu ya kuandika uzi huu unaomlaumu mkuu wa mkoa kumsifu raisi.

Kwao wao mtu anaeandika uzi za kuisifu Chadema au Mbowe kila siku hawezi kulaumiwa, lkn ukimsifu kiongozi yoyote wa serikali lazima ulaumiwe, japo lawama zao hazijawahi kuwasaidia chochote katika chaguzi mbali mbali.

Mleta thread na yeye ni miongoni wa wanaoishi kupitia mfuko wa mwenyekiti wa Chadema.
 
Hahahaha.. wengi wao matusi, majungu na fitna ndio ajira yao. Yani wanalipwa kulingana na aina ya tusi, fitna au majungu utakayoandika hapa JF. Hata mleta uzi huu tayari ana uhakika wa kulipwa kwa sababu ya kuandika uzi huu unaomlaumu mkuu wa mkoa kumsifu raisi. Kwao wao mtu anaeandika uzi za kuisifu Chadema au Mbowe kila siku hawezi kulaumiwa, lkn ukimsifu kiongozi yoyote wa serikali lazima ulaumiwe, japo lawama zao hazijawahi kuwasaidia chochote katika chaguzi mbali mbali. Mleta thread na yeye ni miongoni wa wanaoishi kupitia mfuko wa mwenyekiti wa Chadema.
Hata akina jinga lao wanasifu upande ule mwingine, hii haiondoi ukweli Makalla sio mtu makini,viatu alivyovaa hamvimtoshi
 
Hahahaha.. wengi wao matusi, majungu na fitna ndio ajira yao. Yani wanalipwa kulingana na aina ya tusi, fitna au majungu utakayoandika hapa JF. Hata mleta uzi huu tayari ana uhakika wa kulipwa kwa sababu ya kuandika uzi huu unaomlaumu mkuu wa mkoa kumsifu raisi. Kwao wao mtu anaeandika uzi za kuisifu Chadema au Mbowe kila siku hawezi kulaumiwa, lkn ukimsifu kiongozi yoyote wa serikali lazima ulaumiwe, japo lawama zao hazijawahi kuwasaidia chochote katika chaguzi mbali mbali. Mleta thread na yeye ni miongoni wa wanaoishi kupitia mfuko wa mwenyekiti wa Chadema.
Majina mengine Yana athari Kwa watumiaji wake,hii ni Kwa mujibu wa utafiti wangu mdogo humu,hasa Kwa wanazi wa chukua chako mapema.(ccm)
 
Kuna mtu anaitwa Kunenge mkoa wa pwani. Huyu sijui akifika ofisini anashika faili gani?
Amejaza mabango ya picha yake na ya rais barabarani sijui anadhani yeye ni handsome?
Watu wa Dar, njooni mchukue mtu wenu.
Basi huyo ni mnenguaji na ni mnenga kama wanenga wengine.
 
Majina mengine Yana athari Kwa watumiaji wake,hii ni Kwa mujibu wa utafiti wangu mdogo humu,hasa Kwa wanazi wa chukua chako mapema.(ccm)
Wanasema mtoto wa haramu hata ukimtia ndani ya chupa lazima ataonekana tu.

Sasa umeamua kuonekana na kuonesha upumbavu wako hapa jukwaani. Naona umekuwa na uchungu sana na Mbowe kuliko mke wa Mbowe mwenyewe.

Haya pambania na ww bahati yako ili upewe hata kazi ya kulamba viatu kama wenzako.
 
Back
Top Bottom