Kuna wakati wanaume naomba mtuelewe....

Kuna wakati wanaume naomba mtuelewe....

jaqfantasy212

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2012
Posts
542
Reaction score
258
habari wanajamvini...

ningependa leo niwaombe wanaume watuelewe kama mlikuwa hamtujui, zaidi nazungumza na wanaume walio kwenye mahusiano, unaweza umkuta mpenzi wako amenuna na usijue kilichomfanya anune ni kitu gani, ukweli ni kwamba yeye sio chizi mpaka aamue kununa bila sababu ya msingi, mfano:unaweza ukawa umemuudhi kwenye maongezi yako na wewe usijue kama kuna sentensi ilimkera wakati unaongea na yeye akasindwa kusema kama umemboa kwenye maongezi yako matokeo yake unamkuta mtu amenuna....tafadhali wababa na wakaka unapoona hali ya hewa imebadilika ni wajibu wako kumuuliza mwenzi wako katika hali ya upendo tatizo ni nini, na yeye atakwambia, mtaombana msamaha yataisha na mtaendelea na maisha yenu... kumbuka mwenzi wako anahitaji sana upendo wako unapozungumza naye katika hali ya upendo, anaona unamjali na kumthamini....

ni hayo tu kwa leo....
 
Haya. Usiku mwema.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aisee!
Vumilia dada, ndiyo kilimwengu!

Inagharimu mwanaume aliye balanced kichwani kuanza kumuuliza binti wa mtu, mkubwa mwenzio kuwa umenuna nini, maana nadhani yeye pia ana wajibu wa kuanza kuniambia lililomsibu kabla ya kuchukua maamuzi ya kununa.
 
Aisee wale waleee!!

Hapo ndio tunasema wanawake munguwenu alikufa kwanini unune badala ya kuniambia? Ukinuna itakusaidia nn mwishowe unajizeesha tu.
 
ujumbe umepokelewa tutaufanyia kazi.
 
Watoto ndio wananuna na sio mtu mzima na akili zake,saa zingine mnapenda kubembelezwa sehemu ambayo haina faida,why kama nimekosa unune baada ya kuniambia then tuna move on??utoto mwingine naona kununa nuna....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Hapa ndio utajua umuhimu wa kuongea! Hata wewe kama umekerwa na mwenzio ni muhimu kumwambia kuwa amekukwaza ili ajue!
 
habari wanajamvini...

ningependa leo niwaombe wanaume watuelewe kama mlikuwa hamtujui, zaidi nazungumza na wanaume walio kwenye mahusiano, unaweza umkuta mpenzi wako amenuna na usijue kilichomfanya anune ni kitu gani, ukweli ni kwamba yeye sio chizi mpaka aamue kununa bila sababu ya msingi, mfano:unaweza ukawa umemuudhi kwenye maongezi yako na wewe usijue kama kuna sentensi ilimkera wakati unaongea na yeye akasindwa kusema kama umemboa kwenye maongezi yako matokeo yake unamkuta mtu amenuna....tafadhali wababa na wakaka unapoona hali ya hewa imebadilika ni wajibu wako kumuuliza mwenzi wako katika hali ya upendo tatizo ni nini, na yeye atakwambia, mtaombana msamaha yataisha na mtaendelea na maisha yenu... kumbuka mwenzi wako anahitaji sana upendo wako unapozungumza naye katika hali ya upendo, anaona unamjali na kumthamini....

ni hayo tu kwa leo....

tuwaeleweje wakati nyie kuna muda hamueleweki???
 
Aisee!
Vumilia dada, ndiyo kilimwengu!

Inagharimu mwanaume aliye balanced kichwani kuanza kumuuliza binti wa mtu, mkubwa mwenzio kuwa umenuna nini, maana nadhani yeye pia ana wajibu wa kuanza kuniambia lililomsibu kabla ya kuchukua maamuzi ya kununa.

mkaka mahusiano hayana hizo, hata mm naweza nikakuuliza endapo nitaona haupo sawa...
 
Mwingine ananuna ukimuuliza shida nini anaendelea kukaa kimya mimi nifanyeje sasa hapo? Katika hali hii uwa nachoka naweza kukupotezea hata wiki nzima mpaka umalize masaibu yako mwenyewe.
 
Hapa ndio utajua umuhimu wa kuongea! Hata wewe kama umekerwa na mwenzio ni muhimu kumwambia kuwa amekukwaza ili ajue!

usisahau wanawake tuna tatizo la aibu, isitoshe kuongea naye haitakubadilisha status yako zaidi atakuona ni mwanaume unayejali hisia zake, msiishi kwa mazoea..
 
We nuna tu watu tuelekee bar tukirudi tunalala tu, hasira zikiisha tutaongea
 
Watoto ndio wananuna na sio mtu mzima na akili zake,saa zingine mnapenda kubembelezwa sehemu ambayo haina faida,why kama nimekosa unune baada ya kuniambia then tuna move on??utoto mwingine naona kununa nuna....

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

kwenye mapenzi hakuna utoto, mbona cha nyuma wakati unamfatilia awe mwanamke wako ulikuwa unajishusha, usilete ubaunsa kwenye mahaba....
 
We nuna tu watu tuelekee bar tukirudi tunalala tu, hasira zikiisha tutaongea

mkeo ni mkeo tu, kama bia zingekuwa za maana si ungezioa mbona ulimuoa yeye, mkeo ni mama yako wa pili si vibaya ukawa karibu yake kama yeye anavyokujali kwa kukupikia na kukufulia...
 
Wanaume wengine akili zao sio timamu bidada, hawajajifunza kipi kinafaa kuongea na kipi hakifai.
Kipi cha kumwambia mtu mwingine na kipi hakifai kumwambia mtu mwingine.
Kipi cha kumfanyia mtu mwingine na kipi si kizuri kumfanyia mtu mwingine.

Poleni wanawake, na vile ubongi wa mwanamme ulivo ubwa ni ngumu kuelewa kununa kwa mwanamke. Kununa kwenu ni kazi bure.

Dawa yake mwanamme akifyatua ujinga wake, wewe mwanamke unalipua, ndio ataelewa haukupenda kile alichosema/fanyana siku ingine hatorudia tena.
 
Mwingine ananuna ukimuuliza shida nini anaendelea kukaa kimya mimi nifanyeje sasa hapo? Katika hali hii uwa nachoka naweza kukupotezea hata wiki nzima mpaka umalize masaibu yako mwenyewe.

unaweza ukamuuliza shida nn wakati upo bize na shughuli zako hata yeye kusema shida ni nini hawezi kusema...
 
Back
Top Bottom