Ramon Sanchez
JF-Expert Member
- Oct 9, 2022
- 767
- 1,829
Mambo vp jamiiforums
Ninaandika mada hii sio kama ninahitaji something in return kama vile nipewe pesa au ajira serikali. Hapana. Ninaandika fikra zangu tu kama inavyoona inafaa.
Ndugu zangu, hii nchi bado ni masikini saaana ukilinganisha na nchi kama China, USA, Russia pamoja na England. Kuna baadhi ya mambo tunapaswa kuwakosoa viongozi ila kuna mengine ukijaribu kutizama katika jicho la kibinadamu, utagundua tu ya kwamba hili suala lipo nje ya uwezo wao kwa sababu ya umasikini wa nchi. Pesa haitoshi kuigawa katika familia ya Tanzania kila mmoja aridhike.
Kuna wakati tuwakosoe viongozi lakini wakati mwingine tuwe na aibu kidogo kama ambavyo katika familia unakuta wiki nzima watoto wanakula wali mara moja kwa wiki ndivyo inavyotokea katika ngazi hizi za uongozi wa juu (mishahara kuchelewa, malimbikizo ya madeni, renderers kutokulipwa kwa wakati) haya yote ni dalili ya umasikini wa nchi yetu ya Tanzania.
Kwa kiandika hayo juu simaanishi kwamba hakuna uzembe wa baadhi ya watendaji wachini pamoja na waandamizi wa serikali, hapana, uzembe upo, tuendelee kuwasema lakini sisi bado ni masikini sana.
Jenga picha nchi kama Russia. Nchi ya Russia miaka kadhaa nyuma walikuwa wanatumia internet hii ya kawaida kama ambayo Tanzania inatumia lakini wakaamua kujitoa na kuanzisha internet yao.
Unajua kwa sababu gani waliamua kufanya vile? Kwa sababu Russians are rich compared to Tanzania. Laiti kama Tanzania ingekuwa na GDP kubwa kama hizo nchi za Ulaya, basi na sisi tungeweza kuwa na internet yetu pamoja na kurusha satellite huko juu angani, lakini issue ni umasikini wa nchi.
Nepotism, kujuana pamoja na uswahiba upo na ninaomba tuendelee kukosoa lakini tukumbuke sisi ni masikini ndio maana hata baadhi ya shule za msingi hazina vyoo.
Yangu, mimi leo ni hayo tu. Tuendelee kuwakosoa viongozi lakini tukumbuke ya kwamba Tanzania sio Russia na wala sio Marekani, bali sisi ni Taifa la kipato cha chini na siku zote nchi haziwezi Kulingana.