Kuna uwezekano mtu ukajua software na hardware kwa miezi mitatu tu?

Kuna uwezekano mtu ukajua software na hardware kwa miezi mitatu tu?

Naja naja

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
747
Reaction score
1,559
Kuna hii kozi ya cellular phone maintenance inayotolewa na veta kwa miezi mitatu kwa upande wa software na hardware, sasa je swali ni hivi, kuna uwezekano mtu ukajua software na hardware kwa miezi mitatu tu?
 
Kuna hii kozi ya cellular phone maintenance inayotolewa na veta kwa miezi mitatu kwa upande wa software na hardware , sasa je swali ni hivi ,kuna uwezekano mtu ukajua software na hardware kwa miezi mitatu tu?
Kozi za aina hii zinakuwa ni utangulizi tu. Mambo ya msingi. Ukitaka maarifa zaidi itakubidi ujiendeleze huko mbele ya safari. Kama uko mtundu na unayependa kujifunza funza mambo huko YouTube na kwingineko, kozi kama hii inaweza kuwa chanzo cha wewe kujiajiri.

Mwanzoni utahangaika sana lakini baada ya muda utaimudu kazi yako vizuri. Kasome kama kweli umedhamiria ila pia tumia muda wako mwingi kujiongezea utundu zaidi mtandaoni na huko mtaani kama unafahamiana na mafundi wa simu.
 
Kuna hii kozi ya cellular phone maintenance inayotolewa na veta kwa miezi mitatu kwa upande wa software na hardware , sasa je swali ni hivi ,kuna uwezekano mtu ukajua software na hardware kwa miezi mitatu tu?
Kama tangazo lilisema hivyo, basi inawezekana!

Ni sawa na kuuliza, hivi QT kwa masomo ya form 1 na form 2 kwa Mwaka mmoja inawezekana kweli, ilihali wapo watu wanaweza!!
 
Kozi za aina hii zinakuwa ni utangulizi tu. Mambo ya msingi. Ukitaka maarifa zaidi itakubidi ujiendeleze huko mbele ya safari. Kama uko mtundu na unayependa kujifunza funza mambo huko YouTube na kwingineko, kozi kama hii inaweza kuwa chanzo cha wewe kujiajiri...
Kwa hiyo ndani ya hiyo miezi mitatu mtu unakuwa na uwezo wa kujiajiri tayari?
 
Naomba kujua vyuo vya Veta vinavyo fundisha kozi hizi
 
Back
Top Bottom