Uchaguzi 2020 Kuna uwezekano Magufuli hatafanya kampeni Uchaguzi wa 2020

Kwa kebehi za hawa watu hata kama ningekuwa mimi ndo raisi ningeongoza milele ili kuwakomoa tu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Naamini uliyoyaandika hayawakilishi imani yako ila yanasukumwa na mtazamo wa upande wa pili.

Nikushangae tu wewe unayetukuza lugha ya Kiingereza wakati kuna jitihada za kukuza na kukieneza Kiswahili, lugha ya Taifa. Kwa hilo ni dhahiri una wajibu wa kujitambua, kujiamini na kuchukua hatua stahiki.

Kuhusu demokrasia, amini una tafsiri potofu na ni kwa sababu ya mtazamo wako hasi kuhusu Rais na Serikali.

Demokrasia haipimwi kwa kiwango gani wanasiasa wanapanda majukwaani.

Demokrasia ni utawala wa wengi kupitia wawakilishi waliochaguliwa kwa utaratibu uliokubalika. Kwa nchi yetu uwakilishi unaanzia mtaa/kitongoji hadi Taifa. Na wawakilishi wanawajibika, siyo kupanda majukwaani bali kushiriki vikao vilivyoainishwa kwenye Katiba ya JMT, kusikiliza, kupokea na kuwakilisha yatokanayo kwenye vikao vya juu vya maamuzi.

Uchaguzi hauwezi kuhesabika kutokuwa huru pale tu mshindani anapokosa kuchaguliwa na hatimaye kuilaumu Tume ya Uchaguzi. Na isitoshe mazingira ya kuandaa, kusimamia upigaji kura, kuhesabu na hatimaye matokeo kutangazwa yote huwa huru. Palipo na dosari katika mchakato mzima wa uchaguzi, mahakama ziko wazi kusikiliza malalamiko au madai ya aina hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Huna ujualo zaidi ya kupiga siasa mfu.
 
Nimekutekenya kidogo tu lakini ulivyo ' Nyali ' angalia jinsi unavyotokwa na ' Mapovu ' namna hii. Pole sana hadi nakuonea huruma.
[/QUOTE

Kama wewe nilivyokujambisha ukaanza misifa ya kuduwanzi mara sijui mwanaume wa mara, sijui uduwanzi gani.
K
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Naitazama Tanzania ya miaka 15 mpaka 20 iliyopita. Nimejifunza na kushuhudia mengi. Tulikuwa na nchi ambayo ilikuwa na matatizo mengi na makubwa, ni ukweli ulio wazi matatizo tuliyo kuwa nayo kila mtu aliyashuhudia. Hiki kinachoitwa demokrasia leo ndo kilikuwa kiboko kilichotumika kumpiga kisawasawa mwananchi was chini. Hiki kiboko ndo kilichotumika kuhifadhi maharamia serikalini, wauza unga, meno ya tembo, ujambazi, ukosefu wa maji has a dar es salaam, mikataba mibovu ya madini, huduma mbovu muhimbili na kukosekana kwa vifaa muhimu, yapo mengi sana yanayoonekana kwa macho. Tulichokikosa nchi hii miaka mingi siyo hicho kinachoitwa demokrasia. Maendeleo kwanza mambo mengine baadae, rais Bora ni mwenye dhamira ya kutenda mema ya nchi yenye kuonekana mambo ya kupewa matumaini yasiyokuwa na utekelezaji yalishapita. Ahadi na Utekelezaji ni msingi wa uaminifu. Uwezo wa jamaa wa kutekeleza ahadi zake unatosha kumpa trust ya majority, wanaopiga porojo waendelee kutafuta visingizio tu, mwenzenu anaendelea kutenda na kuaminiwa. Mtamkuta ikulu asubuhi na mapema, watakao mchagua ni wengi kuliko wasemaji wa maneno yasiyokuwa na utekelezaji. At the end trust is earned when actions meet words
 
So what is the point here?


Sent using Jamii Forums mobile app
 

tindo
Unachosema ni sahihi kabsaa!
Magufuli kwa hakika ame-prove failure kwenye Utawala Bora(Good Governance).
Ushindi wake wa 58% mwaka 2015 ulimtia kiwewe na hata report zilizoonesha kushuka kwa umaarufu wake/kuchukiwa na Watz kulizidi kumwongezea HASIRA na majibu yake tumeyaona kwenye Uchaguzi wa SM!
Hataki kurudia makosa ya 2015 ya kuambulia kura kiduchu hivo kuumbuka mchana kweupe…!
Ninachokiona ni kwamba coming GE~2020 his next move will be similar to what he played kwenye LG Election. Kama mtakumbuka juzi wameajiriwa WANAJESHI WENGI SANA KWENYE SEKTA ZA UMMA ikiwemo Halmashauri za Mikoa na Wilaya…!
Hizo ni strategies za kujiweka sawa! Lakini Watz lazima wajur kuwa Magufuli amekuwa akipendelea sana kuvaa MAVAZI YA KIJESHI na hili si kwa bahati mbaya! He's sending a message to his opponents and Tanzanians as a whole kwamba AKISHINDWA KWA KURA anaweza kulitumia Jeshi kutwaa nchi as a Coup d'e tat!!
 
Swali fikirishi kwanini ameiambnia dunia kwamba uchaguzi utakuwa huru kipi kimebadirika kwenye tume ya uchaguzi
 
Amefanya kampeni tangu alipoingia madarakani kila siku yuko live kwenye tv hata kwa matukio ya kawaida. Pia.ikumbukww nec ni mali yake binafsi
 
Je, haya maneno yanaenda kutimia? Tusubiri tuone.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…