Kuna uwezekano 2020 kambi ya Upinzani ikawa ni Wapemba watupu!

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Hii inatokana na ukweli kwamba huku bara kambi ya Upinzani inasambaratika kwa spidi ya mwanga, na kufikia 2020 nadhani upinzani bara atabakia Hashimu Rungwe pekee. Tumaini litabaki kwa Cuf Zanzibar na hasa kule Pemba ambako hawajawahi kuyumba kimsimamo!
 
Sawa sasa undeni tume huru na ya haki na uwazi kwa sababu mna uhakika wa ushindi
 
heshima kwenu ndugu zetu wa bara,
tatizo lenu ni urithi alokuachieni mwalimu nyerere, "WOGA NA UNYENYEKEVU" aliwatisha na aliwaaminisha wazee wenu kuwa yeye ndio mwenye nchi, na hakuna mwenye haki au uwezo wa kutoa maoni ambyo yatapingana na maoni yake.

alijenga mfumo wa khofu wa kila anaepingana nae anamuadhibu, hali hii imewafanya watu wa bara kuwa waoga sana na wanyenyekevu kwa bosi wao na sasa mnawarithisha watoto wenu khofu bila ya kujua.

sisi wapemba tumezaliwa ndani ya upinzani na kujiamini,mimi binafsi sikumbuki lini nilianza kuwa mpinzani, nimekulia na kuwa kama nilivyo tu, dhulma naijua na napingana nayo,na haki naijua na ndio nnayoipigania

kwa mtazamo wa haraka haraka viongozi wa upinzani wa kweli kwa bara ni wachache sana,tundu lisu,lema na wengine wachache,lakini wengi wao ni wenye khofu na mapandikizi,na ubaya wa mapandikizi mara zote ndio wanaokuwa na nguvu na maamuzi mwakubwa ya kupelekesha na kuharibu akili za watu wote

wazungu wana usemi huu “The best way to control the opposition is to lead it ourselves.”

jitafakarini sana
 
We we jidanganyu waambie makada wezako WA CCM watuluusu tufanye siasa kama utaongea upuuzi wako uwo

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Mie nnachowaombe chadema kwa Mungu ni angalau wabaki na viti vya ubunge walivyonavyo leo, ila kwenye urais nadhani hata wao mioyoni mwao wanajua kwamba wataambulia aibu!!

Sent from my HUAWEI G510-0200 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom