lufungulo k
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 2,550
- 1,987
Jana nimesafiri toka Gairo kuja Dar, kwa usafiri wa bus (jina kapuni) katika usafiri ule niligundua usafirishaji wa mabinti wa rika mbalimbali kuja mjini kwa ajili ya kazi za uyaya.
Wengine ilitilisha hadi huruma maana ni wadogo mno, mpaka kuzusha mijadala ndani ya bus hilo. Alijitokeza mama mmoja yeye alimuomba namba mmoja wa binti mdogo ambaye alikuwa akipelekwa kuanza ajira mpya na kuahidi kumpigia huyo mama aliyekuwa ajenti wa hivyo vibinti.
Wale wafanyakazi wa bus nao wanamchango wao mkubwa katika hili, wao hukabidhiwa na madalali walioko chimbo ambao huwafikisha mabinti hao na kuwakabidhi kwa makondakta na kuwapa namba za simu za wale watakao wapokea.
Ni zoezi linalofanywa kwa ustadi mkubwa, kila anapokaribia kushusha mtu, simu zinapigwa mapema na kumkuta anayepokea tayari kituoni.
Mwisho pale Mbezi Magufuli Terminal ndo utasikia tangazo la kondakta. Binti anayetegemea kupokelewa asishuke kwenye bus.
Ushauri: Mabinti hawa wasipandishwe kwenye mabus, bila kuwa na barua za watendaji zenye kuonesha jina, umri , wake, wazazi wake, namba za simu, nida na zikieleza anakwenda wapi? Kufanya nn? Ili kuokoa wale mabinti wadogo kiumri kuzolewa na janga hili.
Tunapiga vita, ushoga, wizi, ubakaji, ufisadi na maovu mengi yafananayo na hayo na kuacha janga hili ni unafiki. Na wanafiki mshahara wao ni motoni.