Kuna umuhim wa afande Nzowa kuchunguzwa

Kuna umuhim wa afande Nzowa kuchunguzwa

skunk

Senior Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
166
Reaction score
27
Habari zenu wakuu, maana ukitaka kutafuta nyoka anzia miguuni mwako, binafsi natia Shaka mwenendo wa ofisa wa polisi kitengo cha madawa ya kulevya bwana Nzowa naona naye pia kama ni mmoja wao hata maamuzi ni ya kutetea mapapa kwa Kuwa busy na dagaa
 
yaani nilivyoangalia na kusikiliza majibu yake live kwenye kipindi cha malumbano ya hoja cha ITV, nikajiuliza kama kweli huyu ndiye aliyepewa dhamana na nchi hii kushughulikia masuala nyeti kama haya, alikuwa too defensive especially kwa maswali mazito toka kwa watu wa aina ya akina Aweda waliokuwepo.
 
Jaribu kufanya uchunguzi wa upatikanaji wake kwenye hiyo nafasi kama si wapoti chukua nafasi hii, au tumesoma wote, tumetoka mkoa mmoja au ndiye ofisa aliyesoma sana kuliko wale wengine pale HQ
 
huyo lazima awe anapeleka fingu la watu waliomuweka pale !!wanawakamata wabeba unga wale waliowatuma hawakamatwi wakati wanajulikana!!!Mwakyembe piga chini nzowa !!!
 
Habari zenu wakuu, maana ukitaka kutafuta nyoka anzia miguuni mwako, binafsi natia Shaka mwenendo wa ofisa wa polisi kitengo cha madawa ya kulevya bwana Nzowa naona naye pia kama ni mmoja wao hata maamuzi ni ya kutetea mapapa kwa Kuwa busy na dagaa

Nashangaa kwa nini hajang'atuka mpaka sasa hivi! Manake kitendo cha kazi yake kufanywa na waziri Mwakyembe kinaonyesha kuwa Nzowa ni mzembe katika utendaji wake! Asisubiri tume ya uchunguzi dhidi ya utendaji wake mbovu iundwe!
 
tunajisumbua bure kutaka mtu mmoja mmoja ang'atuke kwa uzembe,hapa ni kuung'atua mfumo wenyewe tu 2015,mfumo mzima huu ni rotten toka juu,we ushangai maafisa wa usalama wanne kuusishwa na kupitisha madawa but jitu lipo kimya tu,linasoma upepo ndo liseme.watoto wetu wanaangamia wao wanajikosha kwa kuangaika na tiba ya mtu mmoja moja.piga chini ccm,hao ndo wanufaikaji na madawa.
 
Back
Top Bottom