Kuna Ulazima Wa Team Zetu Zote Za League Kuu Kuwa na Kitengo Cha Protocol.

Linguistic

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
3,671
8,237
Nasikia kadhia ya Biashara United, bado hatuna taarifa rasmi kuhusu mchezo wa pili dhidi ya hao walibya,

Vyovyote iwavyo, Kuna siku nliandika, au nlisema katika mahojiano baada ya ile kadhia ya visa kwa safari ya Djibouti, kwamba kama ambavyo Club zina wasemaji/maafisa habari, zinahitaji pia watu wa Protocol ambao kazi yao kubwa ni kudeal na ishu za protocol na logistics.

Mimi nimefanya kazi Foreign Affairs, kuna idara inatwa Protocol Department na pia kuna Idara ya Maadhimisho Ofisi ya Waziri Mkuu, afu kuna Idara/Kitengo cha Maafa pia OWM, walioweka hizo idara walijua umuhimu wake kimajukumua.

So club lazima ziwe na watu wa Taaluma hizo, ambao wao watafanya kazi kama vile kushughulikia passports za kusafiria za Wachezaji na bench la ufundi.

Pale ambapo itahitajika visa watashughulikia kwa wakati, pale itakapohitajika aircraft clearance watawajibika wao nk

Niwape mfano, ikiwa Ndege inakuja nchini ambayo sio commercial flight lazima iombe Kibali Mamlaka ya Anga-TCAA na Ngome.

Haya yote yanahitaji MTU mwenye hiyo taaluma na uelewa wa masuala hayo.

Kufupisha, itoshe tu kusema kuwa, kadri mpira wetu unavyokua be it domestically or internationally, kuna vitu hatuwezi kukwepa.

Tujipange, tusipojipanga tutapangwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubali ushauri. Lakini tunaomba organization structure ya timu ya Biashara tujiridhishe kuwa hakuna kweli kitengo kinachohusu masuala haya. Isije ikawa kuna mtu anavuliwa kengere shingoni na uzi huu.
 
Issue ya Biashara United imenisikitisha Sana, serikali ili handle swala lake kisiasa sana
Mkuu
Mara nyingi wakat wa safar aliepo mbele huwa anasaidia kutoa Taarifa na msaada kwa waliopo nyuma yake, sasa najiuliza msaada wa alie mbele ni upi?

Mana suala la biashara kuwa na ukata ni la muda mrefu lakin walio mbele wamekuja na ratiba za ndege na utaratibu wa kibali cha anga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu
Hivi Baada ya Msimu kwisha kuna jitihada Wana Biashara Mara walifanya na kufanya follow ups pamoja na ushirikishaji?

Kuna Mahusiano ya aina gani baina ya vilabu na vyama vyao vya soka mkoa?

Baada ya Mechi ya Nyumbani wana biashara Mara walifanya nini kuhakikisha logistics za kufika Libya zinatimilika?

Kuna namna Vilabu vinajua maana na umaana wa Mchango wa Serikali katika michezo na kuwashirikisha?

Sasa si nilisikia Biashara Utd walikana hawana changamoto baada ya ule ushindi wa magoli jadid toka kwa Mafie na Atupele? Leo kunani?

Tumezoea kucheza soka letu la ndani kwa maandalizi ya kuzima moto ila tukasahau kule ni michuano ya Vilabu Afrika wajomba.

Katika dunia ya soka la kisasa , klabu haitazamwi kwa Safu ya Benchi la ufundi, Wachezaji na Yafanyikayo uwanjani pekee.

Hivi sasa vilabu ni taasisi na majukumu yake hupangwa annually and semi annually na majukumu yake ya kiutendaji ni 24/7 mwaka mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si nilisikia Biashara Utd walikana hawana changamoto baada ya ule ushindi wa magoli jadid toka kwa Mafie na Atupele? Leo kunani?
Changamoto za fedha walikuwa nazo kitambo tu sema viongozi wao hawakuwa wazi.
 
Back
Top Bottom