Kuna Ukweli gani juu ya mafuta na maji ya upako?

Siku yakikupata, ukaenda Hospital wakasema hawaoni Ugonjwa, ukaenda kwa Waganga wakashindwa.... Ndo utajua Umuhimu wa Imani na maombi....

Umenena yoote..... unakuta unauamwa unafanya mavipimo hospital tofauti tofauti unaambiwa hauna ugonjwa au unachoumwa hakiendani na unachojisikia...... hapo ndio utajua dunia ina pande mbili
 
Haya masuala mengine ni imani tu, hivyo kuamini au kutoamini hutegemea na mtu husika, ila kwa uthibitisho unaweza kwenda kupata maombi au mpeleke ndugu yako wa karibu mwenye changamoto akipata nafuu utakuwa umethibitisha. Ila hizi za runinga ni ngumu kuamini sababu wanaoigiza ni wengi.
Haya
 
Sijapinga maombi Wala nn hoja ni hayo mafuta
Mafuta bila Imani ni bure.....mimi ninaye Dada angu huko shamba yalimkuta yakumkuta, Hospital hazikumsaidia, Waganga hawakumsaidia, binafsi nikamtumia Maji na Mafuta, nikamweleza Imani yake ikiwa juu bila chembe ya Shaka + Maombi + Mafuta/Maji, vitamsaidia...

Alitumia na Maajabu yaliyotokea Mungu shahidi, Sasa ni Mzima!

Unawezaje kumwambia Dada angu huyu kuwa Mafuta/Maji ya Upako sio Chochote akakuelewa!!!
 
It depends na nia ya alieyatoa. According to bible kuna sehem Paulo alihudumu watu walikuwa ni wengi akawaagiza walete maji mafuta vitambaa watu wakawa wanapona kweli. Yesu pia alimponesha mwanamke alietokwa damu miaka 12 kwa kushikwa nguo yake tu. So kikubwa ni kuangalia matendo ya mtu anaetoa hayo mafuta kma ni mpure hakuna shida. Bible inasema mtawatambua kwa matunda yao.
 
Sijasema mafuta ya upako si chochote
 
Amen
 
Binafsi naona kuna loophole moja inatumika. Ukipona utaambiwa mafuta. Usipopona utaambiwa huna Imani vizuri. Kwa hiyo utoboe usitoboe majibu utakutana nayo ni hayo.

Mfano kuna mchungaji mmoja hapa TZ alifanikiwa kufufua mtu, lakini yule mtu baada ya kufufuliwa nilitegemea afatwe ahojiwe aelezee hata ilivyokuwa, imekuwa kimya mpaka leo wakati ilibidi vyombo vya habari vimuandame.

Cha ajabu mwenyekiti alivyoaga dunia hakuonesha hata nia ya kutaka kumfufua.

Kimsingia nimejifunza suala linalohusu Imani halinaga majibu yanayojitosheleza kusema mkafikia tamati ya mjadala husika.
 
Hao ni wajasiliamali wa imani, wanachokifanya ni kuhakikisha wanapata wafuasi wengi kadri inavyowezekana ili wapige mpunga wa kutosha waweze kuishi maisha mazuri, na kupata vitu wanavyohitaji maishani kwao, kwa mfano kuwa na nyumba nzuri, kuwa na usafiri classic, na kung'oa mademu wakali ili wawe mama wachungaji. Sijawahi msikia hata mmoja wao amekwenda hospitali yoyote kufanya miujiza ili wagonjwa wapone. Kama ni kweli tunachokiona kwenye tv kwenye programmes zao ndicho uhalisia kuwa wanamuombea kiwete mpaka anatembea yeye mwenyewe, basi wangeenda kuweka kambi pale wodi ya mwaisela hospitali ya muhimbili ambayo imejaa madereva bodaboda wengi waliovunjika miguu wakiwa wamefungwa antena miguuni, wakapige maombi mazito pale na kuwapaka mafuta na maji ya upako ili kila dereva wa bodaboda anyanyuke adandie bodaboda yake asepe zake nyumbani akiwa mzima wa afya.
 
Imani ngumu Sana, tutafika kwa tabu Sana mbingn
 
Umeongea kwa hisia sana
 
Back
Top Bottom