Kuna ukimya na utulivu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Ule mwangwi wa kile kishindo haujajibu bado. ili uwe mwangwi lazima kuwe na mshindo nyuma

Kaya imeshurutishwa kukaa kimya kwa lazima lakini sio tulivu. Mafikara yanawasokota ndani kwa ndani na fukoto ni kubwa.

Utulivu huleta ukimya, lakini ukimya kamwe hauwezi kuleta utulivu ndio maana Waswahel wanasema kimya kingi kina mshindo mkuu.
Ni kama vile kaya iko kwenye kipindi cha mpito cha sintofahamu kubwa.

  • Wakuropoka wameropoka
  • Wakuongea wameongea
  • Wa kushauri wameshauri
  • Wa kutabiri pia na hata wale wa ramli chonganishi, wote Nolan

Hii ni jamhuri next level. Ukimya uliopo si wa kawaida kiasi kwamba hata wanakaya sasa wanaogopa hata kunong’onezana yatokanayo kunaogofya! Kunatisha sana.

Hebu tuzoeeni kuishi kwa ukimya hata kama hatuna utulivu ili maisha yasonge. Ukimuona fulani karopoka ropo na bado anadunda na hata kugongea veve. Makinika sana. Usiige tembo kunya utapasuka msamba wahenga walisema.
 
Back
Top Bottom