Kuna uhusiano gani wa Damu na masuala ya imani katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaisha?

Maisha ya hapa Duniani yana siri nyingi sana na yanaonekana kuwa na uhusiano wa Moja kwa moja au niseme Connection na ulimwengu mwingine ambao ni wa siri sana yaani ulimwengu usio wa hadharani.

Katika imani nyingi damu imekuwa ikitumika kama kichocheo cha matatizo au kitatuzi cha matatizo. Kwa maana ya kwamba ili umkomeshe adui yako kupitia ulimwengu wa siri damu ya kiumbe hutumika ili kummaliza au kama una tatizo unataka litatuliwe basi damu hiyohiyo ya kiumbe hutumika.

Mathalani, kuna watu hutoa kafara za wanyama ili kufanikiwa kimaisha na wengine huenda mbali zaidi kutoa binadamu kabisa ili kufanikiwa ama kutajirika. Kafara za wanyama au binadamu huhusisha Damu. Na hii hata kwenye Biblia kuna maandiko mengi tu yahusuyo kafara jina lingine zikijulikana kama sadaka za kuteketezwa.

Lakini pia imani ya Kikristo inaamini Damu ya Yesu nayo ni Kitatuzi cha matatizo ya binadamu na ndio damu yenye thamani zaidi kuliko ya kiumbe chochote, yaani ni damu ambayo haihitaji damu nyingine yoyote ili kutatua matatizo au kufanikiwa kimaisha kwa ufupi DAMU ya Yesu Kristo katika imani ya Kikristo ndio Kafara kuu ama Sadaka kuu.

Sasa hapa neno kafara ni Sadaka ya Kishetani kwa mujibu wa imani za kipagani na Sadaka ni ya Kimungu lakini vyote huashiria Sacrifice.

Sasa mimi nauliza kwani huwa kuna uhusiano gani wa kiimani kuhusu Damu na utatuzi wa matatizo ya kimaisha?
Huwa Nina Imani Sana na bro Mshana Jr
Kwenye upembuzi wa haya maswala,nimejifunza na kuepuka mengi kupitia yeye
 
Kwenye ulimwengu wa roho Luna kanuni na hizo kanuni zinafanana maana zina Namba za siri.Mfano kutoa kafara ya damu maanaake Mtu anatengen ezwa na damu
 
Back
Top Bottom