Kuna uhusiano gani kati ya Nyoka na Mapacha

Lukosomolo

Member
Nov 21, 2014
56
12
Ndugu wanajamvi,

Nashindwa kutambua kuna mahusiano gani kisaikolijia, kiimani, ama kwa njia nyingine yoyote ile kuwa nyoka hata awe na mbwembwe kali kiasi gani wala sumu hata angekuwa mkubwa kiasi gani lakini hawezi kumdhuru mapacha ( 2 na zaidi waliokaa ndani ya tumbo 1 la mama na kuzaliwa pamoja) hiyo inawajumuisha wazazi wote wawili yaani baba na mama.

Nyoka hawezi kuwadhuru na hata kama wakionana (Nyoka na Mapacha) Nyoka hunyweaa na anaishiwa nguvu kabisaa na Pacha huweza kufanya lolote alitakalo bila madhara yoyote.

Naomben tujuzane wadau na wataalam kuna nn kati ya hayo mambo mawili?
 
Hii sijawahi sikia mkuu japo mara nyingi watoto ni malaika Mungu anawaepusha na mabaya ,Ile meli ya Nungwi alikutwa mtoto anaelea baharini,jana sijui Geita mama alipigwa na radi hadi kufa na mtoto aliyekua amemshika ni mzima kabisa
 
Hii kitu ishanitokea aiseeee.
Mshana Jr karibu huku uje utoe elimu.
 
duuuuh hata mimi nlishasikia kipindi fulani hivi..ila ilikuwa sio mapacha ni mtoto mdogo tu.
 
Hii sijawahi sikia mkuu japo mara nyingi watoto ni malaika Mungu anawaepusha na mabaya ,Ile meli ya Nungwi alikutwa mtoto anaelea baharini,jana sijui Geita mama alipigwa na radi hadi kufa na mtoto aliyekua amemshika ni mzima kabisa
Kuna mapacha wameshakua tayari. Na wengine wamezeeka. Nashauri tuondoe wazo la malaika.
 
Tujaribu kuwashilikisha watu wazima hasa waliotuleta duniani hao pia wanaweza kuwa dawa maana majibu yetu sisi vijana hayaridhishi
 
Labda kumbukumbu isiwe nzuri.

Nilipokuwa mdogo.

Kama nilishawaiwahi kusikia kuwa nyoka huwa hamdhuru mtoto mchanga/mdogo.

Kuhusu Mapacha sifahamu
 
Back
Top Bottom